Pesa zilivyoweka rehani maisha ya vijana watano
- Ni katika filamu ya Filamu ya the Army of Thieves inayohusu kikundi cha wezi waliobobea kuibia mabilionea.
- Mapenzi yanaingilia kati na kuleta mgawanyiko kwenye kikundi hicho.
SIKILIZA SIMULIZI YA FILAMU YA “THE ARMY OF THIEVES” HAPA
Dar es salaam. Je, unaweza weka maisha yako rehani kwa ajili ya pesa?
Wakati unafikiria jibu la swali hilo, basi ngoja nikukutanishe na kikundi cha wezi kwenye filamu ya “The Army of Thieves” ambao wanayaweka maisha yao rehani kwa kufanya wizi wa hatari kwa bilionea Bly Tanaka mwenye pesa za kumwaga au tunapenda kumwita “fogo”.
Wizi wanaofanya watu hawa siyo wa kutumia nguvu sana, bali ni akili na ufahamu wa teknolojia kwa sana huku umakini wa hali ya juu ukiwapa polisi wabobezi ugumu wa wa kuwatia hatiani.
Ukubwa wa kazi inayofanywa na watu hawa unaweza kufikiri ni kundi kubwa la watu, kumbe ni watu watano tu, wanaoongozwa na mwanadada mrembo Gwendoline ambye unaweza kudhani ni “Slayqueen” tu asiye na baya, kumbe ni kinyume chake.
Gwendoline, alianzisha kikundi hicho na watu watatu, Korina (mdukuzi matata), Roph (dereva) asiyeogopa ajali pamoja na Brad mpiganaji wa kikundi hicho ambaye pia ni mpenzi wake na Gwendoline.
Wote hawa ni wahalifu sugu ambao kila mamlaka ya usalama inawasaka.
Kwa kazi wanayotaka kuifanya, inahitaji mtu mwenye ubobezi wa kufungua loki za vifaa vya kuhifadhia nyaraka na vitu vya thamani (safe). Tofauti na safe ulizozizowea, ninazoziongelea hapa ni za mtu ambaye aliwekeza maisha yake yote kutengeneza safe hizo.
Kuzifungua, unahitaji kujua historia, kuwa na sikio la kusikia hatua za sisimizi na akili ya kupembua saikolojia.
Mtu huyo ni Sebastian. Mtaalam wa kufungua , bila kuvunja wala kuharibu safe zilizodizainiwa na mtaalamu Hans Wagner.
‘Mission’ za pesa
Uwepo wa Sebastian kwenye kikundi hiki, unafanya waanze kujiamini na kuweka mipango ya kuiba pesa katika Safe za Tanaka, mpango ukiwa ni kuiba katika safe tatu zilizojaa mijihela na wakimaliza basi watamuondoa Sebastian kwenye kikundi chao.
Mission ya kwanza inakuwa ni kufungua safe ya pesa iliyopo katika moja ya bank kubwa kwenye jiji la Paris nchini Ufaransa.
Cha kufurahisha ni kwamba nia yao si kuiba vitita vyote vya pesa vilivyopo katika safe hiyo, ila awamu hii wanachotaka ni kuacha alama tu au wenzetu husema ‘legacy’.
Lengo lao linapofanikiwa wanandaa mission ya pili ambayo ni ngumu kuliko ya kwanza na cha zaidi ni kwamba wakikosea tu kuifungua safe hiyo basi itajifunga milele.
Nikwambie tu wakati hayo yote yakiendelea Sebastian anaanza kumpenda Gwendoline bila ya kujua kwamba mdada huyo ana mahusiano ya kimapenzi na Brad.
Hisia za Sebastian kwa Gwendoline, zinaleta uadui kwenye kikundi hicho, hasa pale Brad anapogundua kuwa wawili hao wameanzisha ukaribu usio wa kawaida.
Mgawanyiko na chuki vinatokea kabla hata ya mission kuisha ambapo Gwendoline, Sebastian na Korina wanakuwa kundi moja huku Brad na Roph wakichukua njia yao totauti.
Safe zipo tatu na hadi sasa zimefunguliwa mbili. Nani atawahi kufungua safe ya tatu? Ni timu ya Gwendoline au Brad?
Fuatilia meno na ndimi za filamu hii iliyopo kwenye jukwaa la Netflix ambayo inamafunzo mengi lakini makuubwa ni mahusiano, imani na uaminifu.
Umewahi kuijua nguvu iliyopo kwenye kusikiliza? Kama bado basi huenda ukaanza kutilia maanani kwenye kazi ya masikio yako.
Latest