Filamu ya “No Time To Die”: Mashaka yaliyojaa majuto

November 12, 2021 9:36 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inamhusu ”Agent 007” ambaye mashaka kwa mpenzi wake yanabaki majuto ya milele.
  • Umafia mzito wa kulipiza kisasi na misheni za kuukomboa ulimwengu ni sehemu ya filamu hii.

Dar es Salaam. Mapenzi ni kama hisia ya mtoto anapocheza na baba yake. Hata akirushwa juu kwa kiasi gani, imani yake ni kuwa baba atanyanyua mikono na kumdaka kabla hajaanguka chini. 

Tena, ni kama hisia ya mtoto anayeomba pipi kwa mama yake. Hata akiambiwa, “mwanangu nitakuletea kesho”, anaamini maneno ya mama na kuendelea kucheza.

Hata hivyo, bahati ya mapenzi siyo ya wote, Wakati Adamu akikutana na Hawa kwa urahisi, wengine ni Samson wanaoishia na Delila.

Samson wa leo ni James Bond almaarufu kama Agent 007. Huenda ndiyo muuaji mtanashati ambaye umewahi kukutana naye kwenye ulimwengu wa filamu lakini nani alitabiri kama jasusi anayeweza kuchomoa moyo wa mtu huku akimwangalia machoni naye anaweza kudondoka kwenye huba?

Kwa Bond, mdondoko wake unaonekana haukuwa na bahati. Alidondokea kwa mwanamama Madeleine Swan aliyefanya ukuu wa steringi wetu kupotea kama barafu ipoteavyo kwenye maji ya moto.

                   

Filamu ya “No Time To Die” inaanza na wawili hao wakiwa katika mji wa Matera uliopo kusini mwa nchi ya Italia. 

Ni muda wa wawilihao kula bata. Matarajio yao ni kuwa hakuna mtu anayewafuatilia kwani wanaishi maisha yao mbali na rada. 

Hata hivyo, kumbe tayari kuna chui ambaye alikuwa ameshanusa harufu zao.

Wakiwa hawajui hili na lile, Bond na Swan wanajikuta ni “target” ya watu ambao wamedhamiria kuwaua. 

Wanakimbizwa, wanakoswa koswa na pale njia ya kukimbilia inapokoma, wanajikuta wakiwa wamezingirwa tena na watu ambao bastola zao zimewaelekea na siyo kuwaelekea tu, zinamimina risasi zilizowalenga.


Soma zaidi


Kumbuka hapa tunamuongelea Bond. James Bond na kama umekuwa ukifuatilia filamu za 007, unafahamu aina ya magari anayotembelea. 

Kwa gari la leo, halipitishi risasi lakini haliwezi kubaki hivyo hivyo kwa muda mrefu. 

Bond yupo kwenye mawazo mazito akifikiri kama kile kilicho akilini mwake kina usahihi.

Mawazo hayo ni kuwa, amesalitiwa na mwanamke ambaye alimpenda. Mwanamke aliyeacha kila kitu kwa ajili yake. Binti Madeleine Swan.

Kwa hali aliyopo Bond, hasikii la kuambiwa. Licha ya Swan kujitetea kwa kila hali, Bond anamtelekeza Swan na kuanza kutafuta mwanzo wa uzi ulioagiza kifo chake. Asichokijua ni kuwa, Binti Swan alikuwa mbioni kuitwa mama na mtoto huyo, si wa mwingine. Ni wa Bond.

Huenda “No time to die” ikawa filamu ya mwisho kwa Craig kama James Bond. Picha| Cyber Punk Film.

Maisha mapya ya Bond

Miaka mitano baadaye, silaha angamizi inatengenezwa baada ya mwanasayansi Valdo Obruchev kutekwa na kundi la magaidi. 

Silaha hizo zinaitwa nanobots ambazo zinaua kwa njia ya maambukizi kama virusi lakini tofauti na virusi ambavyo tumevizoea. Nanobots zinafanya kazi kwa kuua watu ambao vinasaba vyao vimetengenezwa na silaha hizo.

Misheni ya Bond ni kumuokoa Obruchev lakini safari hiyo ni kama kuku kujipeleka kwenye shimo la nyoka wenye njaa kali. Hivyo huenda maisha ya Bond nayo yakawa kwenye hati hati.

Sijui kama atafanikiwa kurudi au itabidi tuanze kutafuta mwili kwa ajili ya kuzika. Ninachojua ni kuwa unaweza kufuatilia filamu hii kupitia kumbi za kutazamia filamu ikiwemo za Century Cinemax za zingine unazozifahamu kuzijua mbivu na mbichi. 

Kumbukumbu zinazoumiza, Mshaka yaliyojaa majuto, rafiki wanaogeuka adui na “karma” yenye dhamira ya kutimia ni sehemu ya filamu ya “No Time To Die”.

Kutana na nguli wa maigizo, Daniel Craig, Rami Malek, Lashana Lynch na wengine kibao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV