Tanzania yaimarisha mapambano dhidi ya Uviko-19
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imezidi kuimarisha hatua za kupambana dhidi ya janga la corona, ikiwemo mikakati ya kuongeza utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo.
Mikakati hiyo ni pamoja na kuzindua awamu ya pili ya kampeni ya jamii shirikishi itakayoanza Desemba 22 mwaka huu jijini Arusha, ambayo itahusisha watoa huduma ngazi ya jamii zaidi ya 8,130 waliopatiwa mafunzo ya kuelimisha na kuhimiza wananchi kupata chanjo ya Uviko-19.
Hadi Desemba 18 zaidi ya watu milioni 1.28 sawa na asilimia 2.2 ya watu wote Tanzania walikuwa wamekwisha chanja chanjo ya Uviko-19 na kupata kinga kamili.
Aidha Wizara ya Afya imeeleza kuwa visa vya Uviko-19 vinaongezeka kwa kasi na kuwaomba wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono.

Latest
