Tanzania yazidi kupokea chanjo, waliochanjwa wakifikia asilimia 1.7 ya watu wote

November 25, 2021 11:19 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Dozi 499,590 za chanjo aina ya Pfizer zilipokelewa nchini Novemba 23
  • Jumla ya watu 988,293 sawa na asimilia 1.7 ya idadi ya watu Tanzania wamemaliza chanjo ya Uviko-19

Dar es Salaam. Hatua ya Serikali ya Tanzania kupokea awamu ya tatu ya chanjo ya ugonjwa huo aina ya Pfizer dozi 499,590 kutoka Marekani kupitia mpango wa ‘COVAX Facility’ itaisadia katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 unaoendelea kusumbua mataifa mbalimbali ulimwenguni. 

Dozi hizo zilipokelewa Novemba 23, 2021, ambazo zitakinga watu 249,795 kwa dozi mbili, zinatimiza jumla ya dozi milioni 4.3 za chanjo za Uviko-19 ambazo zimeshapokelewa nchini.

Ujio wa chanjo hiyo unazidi kuwapa fursa wananchi kuchagua chanjo wanayotaka kuchanja na kujikinga dhidi ya janga la Corona. 

Hadi kufikia Novemba 11, 2021, jumla ya watu milioni 1.6 walikuwa wamepatiwa chanjo ya Uviko-19 nchini, ambapo kati ya hao watu 988,293 sawa na asilimia 1.7 ya watu wote nchini wamemaliza chanjo na kupata kinga kamili dhidi ya ugonjwa huo, kwa mujibu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 

Hadi sasa mikoa inayoongoza kwa kutoa chanjo nchini ni pamoja na Dar es Salaam, Kilimanjaro,dodoma, Arusha, Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, na Kagera.

Hadi Novemba 24, jumla ya dozi bilioni 7.4 zimeshatolewa katika maeneo mbalimbali duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV