Tanzania yapokea shehena nyingine ya chanjo ya Uviko-19

January 26, 2022 10:55 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi kufika Januari 23, 2022 jumla ya watu 33,000 wamethibitika kuwa na maambukizi ya Corona (Uviko-19) na 781 kati yao wamepoteza maisha  huku Serikali ikiimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Ummy aliyekuwa akizungumza leo Januari 26, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya chanjo aina ya Sinopharm kwa ufadhili wa Serikali ya China jumla ya dozi 800,000 ambazo zitatumika kuchanja wananchi 400,000 amesema watu wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari.

“Naishukuru Serikali ya China kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo hizi awamu ya pili kwa chanjo za aina hii awamu ya kwanza tulipokea jumla ya dozi 500,00 ambazo zilitumika kuchanja watu 250,000,” aamesema Ummy.

Hata hivyo, amesema mwenendo wa utoaji wa chanjo ni wa kuridhisha ambapo takwimu za Januari 25, 2022 jumla ya watu milioni 1,9 milioni sawa na asilimia 3.33 ya Watanzania waliokuwa wamepata chanjo kamili.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW