Hapana: Marekani haibadilishi noti za fedha zake

November 21, 2022 12:55 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakuna uthibitisho wa nchi hiyo kubadili fedha zake.
  • Mpaka sasa nchi hiyo ina noti 7 za Dola zinazotumika shughuli za kifedha.

Dar es Salaam.Siku za hivi karibuni kumezuka taharuki miongoni mwa watumiaji wa fedha za Marekani (Dola) maara baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa Januari 31, 2023 nchi hiyo imepanga kuzuia matumizi ya noti zake zilizotengenezwa chini ya mwaka 2021.

Taarifa hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamiii na baadhi ya vyombo vya habari si ya kweli.

Wasambazaji wa uzushi huo wanadai kuwepo kwa mkutano  uliofanyika Washington DC nchini humo Novemba 5, 2022 baina ya Benki Kuu ya Marekani na mashirika makubwa ya kifedha kama Shirika la Fedha la Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB) jambo ambalo halina uthibitisho.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya kuwepo kwa mkutano wowote wa mashirika hayo kwenye tovuti kuu ya Serikali ya Marekani pamoja na mashirika yanayohusishwa na uzushi huo.

Kwa mujibu wa tovuti ya US currency education programme ya nchini Marekani, mpaka sasa kuna noti saba tu za Dola zinazotumiwa kwenye masuala ya kifedha ya nchi  hiyo.

Noti ya kwanza ni ya Dola moja, mbili, tano, 10,20,50 na 100 na noti ya mwisho kutengenezwa ilikuwa ni Dola 100 iliyotengenezwa mwaka 2013.

Sambamba na hayo tovuti hiyo inasema iwapo Serikali ya nchi hiyo ikafanya mabadiliko ya muundo wa fedha zake bado fedha zilizopo kwenye matumizi katika nchi mbalimbali ni halali kwa matumizi, tofauti na uzushi unaosambaa kwamba hazitatumika tena.

“Ni sera ya serikali ya Marekani kwamba miundo yote ya sarafu ya Marekani itasalia kuwa zabuni halali, bila kujali ilitolewa lini,” inasema tovuti hiyo

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW