Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Februari 3, 2026
Katika viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania vinavyotolewa na Benki za CRDB na NMB kwa matumizi ya leo Februari 3, 2026, Dola ya Marekani imeendelea kuongezeka thamani dhidi ya Shilingi ya Tanzania ikilinganisha na ilivyokuwa wiki iliyopita.
Viwango hivi hubadilika kila siku kulingana na mwenendo wa soko la fedha, na vina umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara, wawekezaji na walipakodi, hasa katika kufanya malipo ya ada, kodi pamoja na ununuzi na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Kupitia viwango hivi vya kubadilisha fedha, watumiaji wa sarafu za kigeni hupata mwongozo sahihi wa kupanga bajeti, kufanya manunuzi na kuendesha shughuli zao za kifedha kwa ufanisi zaidi
Katika viwango vya leo, Dola ya Marekani inanunuliwa kwa Sh2,640 na Benki ya CRDB kutoka Sh2,520 iliyokuwa ikinunuliwa Januari 5, 2026.
Hata hivyo, fedha nyingine kutoka mataifa mengine duniani zimeendelea kuimarika au kushuka kama inavyoonekana ikiashiria mabadiliko ya nguvu ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kimataifa.

Latest