Walimu bado changamoto shule za msingi Maswa

March 18, 2022 1:17 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwalimu mmoja anafundisha takriban wanafunzi 71 katika shule za msingi.

Dar es Salaam. Changamoto ya idadi ndogo ya walimu wa shule ya msingi, imeendelea kuitesa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa iliyopo Mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu Muhimu za Elimu (2021) zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi, wilaya hiyo yenye wanafunzi wa shule za msingi 83,898, ina walimu 1,189 pekee, hali inayosababisha mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 71, kiwango ambacho ni juu ya uwiano wa Kitaifa wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 45.

​Changamoto inaongezeka zaidi kwa walimu wa kike ambao wapo 470 sawa na asilimia 39.5 ya walimu wote wa shule za msingi wilayani humo.

Hali hiyo inasababisha wanafunzi wa kike ambao wameanza kupata hedhi kushindwa kupata msaada wa karibu wawapo shuleni.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV