Corona ipo, chukua tahadhari

June 8, 2022 8:38 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kati ya Mei 5 hadi Juni 3, Wizara hiyo imeripoti jumla ya visa vipya 160.

Dar es Salaam. Wizara ya Afya nchini Tanzania imewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Uviko-19 ikiwemo kupata chanjo kwa sababu ugonjwa huo bado upo.

Kati ya Mei 5 hadi Juni 3, Wizara hiyo imeripoti jumla ya visa vipya 160 ingawa hakujaripotiwa kifo chochote katika miezi miwili iliyopita.

Tarifa hiyo ya wizara hiyo iliyotolewa Juni 7, 2022 imeainisha mikoa ambayo imeripoti kiwango kikubwa cha maambukizi ambapo Dar es salaam imeripoti visa 130, Arusha (10), Mwanza (5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2) na Mara  ni visa viwili.

Waliopata chanjo kati ya Mei 5 mpaka Juni 3 ni 775,680 huku wagonjwa watatu waliothibitika kuwa na maabukizi na kulazwa wote walikuwa hawajapata chanjo hivyo wizara imeendelea kusisitiza wananchi kupata chanjo kamili ya Uviko-19.

Kujikinga na ugonjwa huo, wananchi wametakiwa kupata chanjo, kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV