WHO: Uviko-19 bado upo, unaendelea kuua watu

August 27, 2022 6:34 am · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema watu milioni 1 wamefariki kwa ugonjwa huo.
  • Yasisitiza kuongeza nguvu ya kutoa chanjo. 

Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Tedros Ghebreyesus amesema watu hawapaswi kujisahau wala kuchukulia kama janga la Uviko-19 limeisha kwa sababu linaendelea kuua mamilioni ya watu duniani.

Dk Tedros aliyekuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Geneva Uswisi, Agosti 25 mwaka huu amesema “hatuwezi kusema tunajifunza kuishi na Uviko-19 wakati watu milioni 1 wamekufa na Uviko-19 mwaka huu pekee.”

Amewaambia waandishi wa habari kuwa miaka miwili na nusu ya janga la Uviko-19 duniani “tuna nyenzo zote tunazohitaji za kuzuia vifo vitokanavyo na janga hili.”

Amezitaka serikali zote ulimwenguni kuimarisha juhudi zao za kutoa chanjo kwa wahudumu wote wa afya, wazee, na wengine walio katika hatari kubwa zaidi, mbinu hii ikiwa ni moja katika njia za kuweza kufikia utoaji wa chanjo ya Uviko-19 kwa asilimia 70 kwa watu wote ifikapo Desemba 2022.

“Inafurahisha kuona kwamba baadhi ya nchi zilizokuwa na viwango vya chini zaidi vya chanjo sasa zinainuka hususan barani Afrika,” amesema.

“Inafurahisha sana kuona kwamba utoaji chanjo unazingatia makundi yanayohitajika kupewa kipaumbele huku nchi nyingi zikipiga hatua ya kuvutia katika kutoa chanjo kwa asilimia 100 ya wafanyakazi wa afya na asilimia 100 ya wazee.”

Hata hivyo Dk Tedros amesema bado mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kutokomeza janga hilo la Afya ulimwenguni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV