Uviko-19: Hali halisi ya maambukizi Afrika Mashariki

September 2, 2022 12:22 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kenya kinara maambukizi na vifo vya Uviko-19 Afrika Mashariki
  • Watu wahimizwa kuendelea kuchukua tahadhari.

Dar es salaam. Licha ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya Uviko-19 katika nchi za Afrika Mashariki, bado wananchi wanakumbushwa kuendelea kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo kwa sababu bado upo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hadi kufikia Agosti 31, 2022 nchi ya Kenya ilikuwa imeripoti visa 338,170 pamoja na vifo 5,674 ikiwa ndio nchi  iliyoripoti visa vingi zaidi vya maambukizi pamoja na vifo katika nchi za Afrika Mashariki.

Sudan Kusini imeripoti visa 17,780 vya maambukizi ya Uviko-19 ikiwa ndio nchi iliyoripoti visa vichache zaidi ingawa imeipiku Burundi kwenye idadi ya vifo kwani wamefariki watu 138 ilihali Burundi wamefariki watu 15.

Tahadhari zinazohimizwa kuendelea kuchukuliwa ni kupata chanjo kamili ya Uviko-19, kuvaa barakoa na kutembelea kituo cha afya ikiwa mtu anahisi dalili za ugonjwa huo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV