Muswada bima ya afya kwa wote wakwama tena bungeni

February 9, 2023 9:16 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bunge lasema unahitaji kufanyiwa maboresho.
  • Utawasilishwa katika mikutano ijayo ya Bunge. 

Dar es Salaam.  Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao ulikuwa uwasilishwe bungeni leo umekwama kwa mara nyingine ili kutoa fursa ya kurekebisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana yana upungufu.  

Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameliambia Bunge leo Februari  9, 2023 jijini Dodoma kuwa muswada huo ambao ulikuwa uanze kujadiliwa bungeni leo na kesho, umerudishwa kwenye kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kujadiliwa zaidi.

Dk Tulia amesema muswada wa Bima ya Afya kwa Wote umesogezwa mbele mpaka wakati mwingine ambapo kwa sasa majadiliano yanaendelea na hasa eneo la bajeti na utekelezaji wa muswada huo.

“Sasa hati hii haitawasilishwa leo mezani kwa sababu Bunge pamoja na Serikali tunaendelea na mashauriano juu ya mambo ambayo hatujaafikiana vizuri,” amesema Spika Tulia. 

Hii ni mara ya pili muswada huo kukwama tangu usomwe kwa mara ya kwanza bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge na kupelekwa katika kamati hiyo kwa ajili ya kuchambuliwa.

Hivi karibuni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na watendaji wa wizara yake wamekuwa wakikutana na makundi mbalimbali ya wadau wakiwemo viongozi wa dini ili kutoa elimu na kuongeza uelewa wa bima hiyo na kupokea maoni maeneo ya kuboresha.

Huenda kukwama kwa muswada huo kutapunguza matumaini ya Watanzania kuipata bima hiyo kwa wakati ikizingatiwa kuwa watu wengi wanalalamikia gharama kubwa za matibabu wanapoenda hospitali.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV