Shule za awali, msingi, sekondari sasa kufungwa Novemba 13, 2026

October 2, 2026 9:10 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana na tahadhari ya mvua za Elnino zilizotabiriwa kuanza Oktoba hadi Desemba, 2026.

Arusha. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza tarehe mpya ya kufungwa kwa shule za awali, msingi na sekondari kufuatia tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa za Elnino.

Taarifa ya Kamishna wa Elimu Dk Lyabwene Mtahabwa, iliyotolewa leo Oktoba 2, 2o26 inabainisha kuwa wanafunzi wa ngazi hizo za elimu watafunga shule Novemba 13, 2026 badala ya Desemba 2, 2026 iliyopangwa awali.

“Hatua hii inalenga kulinda usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine katika shule, imesisitiza taarifa ya Dk Mtahabwa.

Wizara ya elimu imebadili tarehe hizo za kufunga shule ikiwa ni wiki sita tangu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) itahadharishe umma  juu ujio wa mvua za El Nino zitakazoanza mwanzoni mwa Oktoba hadi Desemba 2026.

Katika taarifa yake ya Agosti 18, 2026, TMA ilisema mvua hizo zinaweza kuwa juu ya wastani au wastani katika baadhi ya maeneo zikisababisha mafuriko pamoja na uharibifu mwingine wa mali na miundombinu.

Kutokana na tahadhari hiyo, Wizara ya Elimu ilifanya mabadiliko ya tarehe za upimaji na mitihani ya kitaifa ikiwa ni hatua muhimu ya kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na athari za mvua hizo.

Mabadiliko hayo yanafanya mitihani ya Darasa la Nne (SFNA) kufanyika Oktoba 5 na 6 badala ya Oktoba 21 na 22, Darasa la Pili (STNA) Oktoba 7 na 8 badala ya Novemba 17 na 18.

Kwa upande wa Kidato cha Pili (FTNA) wataanza mitihani yao  Oktoba 12 hadi 23 badala ya Novemba 2 hadi 13, huku mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) ikianza Oktoba 19 na kumalizika Novemba 6 badala ya Novemba 9 hadi 27.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
3 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
3 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zingatia mambo haya kabla ya kusaini mkataba wa ajira

Zingatia mambo haya kabla ya kusaini mkataba wa ajira

Nukta TV

Rasmi wageni kuanza kulipa USD44, bima ya safari Tanzania

Rasmi wageni kuanza kulipa USD44, bima ya safari Tanzania

Nukta TV

Hofu yatajwa, kwanini Watanzania wengi hawapimi afya mara kwa mara?

Hofu yatajwa, kwanini Watanzania wengi hawapimi afya mara kwa mara?

Nukta TV