Bima ya Afya kwa Wote kuanza rasmi Januari 26

January 23, 2026 7:05 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Awamu ya kwanza kuanza na makundi maalum ikiwemo wajawazito, wazee na watoto.
  • Bei mpya ya kitita yatangazwa.

Dar es Salaam. Serikali imetangaza kuanza rasmi kwa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Bima ya Afya kwa Wote (BAW) kuanzia Jumatatu, Januari 26, 2026 hatua inayolenga kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wananchi, hususan makundi yasiyo na uwezo.

Akizungumza leo Januari 24, 2026, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa katika kikao kazi cha kitaifa cha kujadili utekelezaji wa mpango huo, amesema bima hiyo itaanza kutumika kwa kitita cha huduma muhimu, kitakacholenga makundi yaliyo hatarini.

Makundi hayo yanajumuisha wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao gharama zao zitagharamiwa na Serikali huku wananchi wa kawaida wakitangaziwa bei mpya ya kitita cha huduma muhimu.

“Bei ya kitita hicho ni Sh150,000 kwa kaya isiyozidi watu sita, kikiwa kinazingatia utaratibu wa rufaa katika vituo vya afya vilivyoingia mkataba na Skimu za Bima ya Afya,” ameongeza Mchengerwa.

Bima ya afya kwa wote ni miongoni mwa mipango iliyokosolewa vikali wadau wa sekta ya afya na baadhi ya wananchi katika mitandao ya kijamii tangu kuwasilishwa kwa mswada wa kwanza wa sheria hiyo bungeni Dodoma Septemba 23,2022.

Tangu mwaka huo mswada huo umekuwa ukikumbana na viunzi vilivyosababisha kushindwa kutekelezeka hata baada ya Bunge kupitisha rasmi Novemba 1, 2023 na kufanyiwa maboresho Februari 12, 2025.

Hata hivyo, Novemba 14, 2025 Rais Samia  Suluhu Hassan aliyekuwa akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza aliahidi kutekelezwa kwa hatua za awali za mpango huo katika siku 100 za uongozi wake wa awamu ya pili.

Hata kabla ya siku hizo kuisha tayari Watanzania wameanza kuona mwelekeo chanya unaoashiria mwanzo mpya wa huduma bora za afya nchini.

Mifumo ya Tehama kusomana

Mchengerwa ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya Tehama ili kuweka kumbukumbu za wagonjwa katika vituo vyote vya afya nchini, hatua itakayosaidia kuondoa urudiaji wa vipimo na kupunguza usumbufu kwa wagonjwa pamoja na mzigo kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

“Mwananchi hapaswi kubaki nje ya mfumo kwa sababu ya urasimu au uzembe wa mifumo. Pale mifumo ilipo na mtu hajasajiliwa, hilo ni tatizo la uongozi,” amesisitiza Waziri.

Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk Grace Magembe, amesema utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote utahakikisha upatikanaji wa huduma za afya, kurahisisha uwezo wa kugharamia huduma hizo na kuboresha ubora wa huduma nchini.

1 thought on “Bima ya Afya kwa Wote kuanza rasmi Januari 26

  1. Binafsi nashukuru angalau mpango huu utasaidia kaya maskini na wenye uwezo mdogo kupata matibabu tofauti na ule wa nyuma ambao kwa vyovyote vile ilikuwa ni vigumu kwa mtu wa maisha ya kawaida kumudu.
    Rai yangu huu mpango serikali ifuatilie kwa kina utekelezaji wake hasa kwenye baadhi ya Hospital bado wanabagua wanapoona mtu anatumia bima na pia serikali iendelee kufanyia kazi kuhusu baadhi ya vipimo na dawa kubaguliwa bado ni tatizo maana unakuta mtu hana uwezo wa kulipa pesa taslimu, Kuna haja ya kuwa na bima ambayo haitabagua baadhi ya vipimo na dawa

Comments are closed.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV