Waziri Ummy: Bima ya afya ni hiari

September 27, 2022 9:01 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema hakuna mtu atakayelazimishwa kujiunga na bima ya afya kwa wote. 
  • Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ikipita itahakikisha wananchi wanapata huduma bila kikwazo.
  • Watu wataweza kuchangia kidogo kidogo. 

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ikipita itahakikisha wananchi wanapata huduma bila kikwazo lakini hakuna mtu atakayelazimishwa kuwa na bima hiyo kwa sababu itakuwa ni hiari. 

Muswada wa sheria hiyo uliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza Septemba 23, 2022 ambapo utajadiliwa katika kamati kabla ya kumalizia mchakato mwingine wa utungaji wa sheria.

Waziri Ummy aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 27, 2022 amesema bima hiyo itakuwa ni hiari siyo lazima. 

“Hakuna mtu atakayepigwa faini, atakayefungwa au kubughuziwa kwa namna yoyote ile kisa hatakua na bima ya afya. Bima ya afya ni hiyari,” amesema Waziri Ummy.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kikwazo na kwa gharama nafuu.

“Tutaendelea kuelimisha kuwa lengo la Serikali kupitia bima hii ni kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wananchi,” amesema Ummy ambaye ni Mbunge wa Tanga Mjini.

Ili kuhakikisha sheria hiyo inatekelezeka vizuri, utawekwa utaratibu wa kuchangia kwa kuzingatia kaya, na mtu mmoja mmoja asiye katika kaya ambapo bima hiyo itakuwa na kitita cha msingi na vifurushi mbalimbali vitakavyowezesha wananchi kuchagua kulingana na mahitaji.

“Kwa wasio na uwezo Serikali itatumia utaratibu wa TASAF(Mfuko wa Maendeleo ya Jamii) kuwatambua kwa ajili ya kuwapa huduma. Wananchi hawatalazimishwa kujiunga na mfuko mmoja, watakua wa na uhuru wa kuchagua skimu za bima zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza Ummy. 

Amesema malipo ya bima yanaweza kuwekewa utaratibu wa kulipwa kwa awamu kulingana na uhitaji wa wateja na watoa huduma. 

Akizungumzia kufungamanisha na baadhi ya huduma za kijamii ni kuongeza msukumo wa watu kuchangamkia fursa hiyo ya kuwahakikishia afya zao. 

“Kufungamanishwa kwa baadhi ya huduma za kijamii kunatarajia kuweka msukumo kwa wananchi ili wachukue hatua za kujiunga na bima ya afya ili kuepuka changamoto ya kutopata huduma za afya bila kikwazo cha fedha,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Serikali inatarajia kufungamanisha umiliki wa kadi ya bima ya afya kwa wote na upatikanaji wa huduma zilivyofungamanishwa na umiliki wa kadi au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV