WHO: Uviko-19 sio tena dharura ya kimataifa

May 7, 2023 5:42 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema ugonjwa huo umepungua katika maeneo mbalimbali duniani.
  • Chanjo na jitahidi za pamoja zasaidia kuudhibiti ugonjwa huo.
  • Yatoa tahadhari watu kutojisahau.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza rasmi kuwa  ugonjwa wa Uviko-19 uliokuwa ukiitesa dunia kwa miaka kadhaa iliyopita siyo ugonjwa wa dharura wa afya ya jamii kimataifa.

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Ghebreyesus aliyekuwa akitangaza uamuzi huo wa kamati ya dharura ya kimataifa ya kanuni za afya (2005) kuhusu janga hilo uliofanyika Mei 4, 2023, amesema ugonjwa huo sio dharura ya kimataifa.

“Kwa matumaini makubwa janga la Uviko-19 limekomeshwa kama dharura ya afya ya umma,” amesema Ghebreyesus.

Uamuzi huo wa WHO umekuja wakati kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 ikipungua huku kukiwa hakuna maambukizi mapya ndani ya saa 24 zilizopita duniani kote.

Kwa mujibu wa WHO mpaka kufikia Mei 3, 2023  kulikuwa na vifo milioni 6.9 huku utoaji wa chanjo ukiwafikia watu bilioni 13 duniani kote.

Viwango vya vifo vimepungua na shinikizo kwenye mifumo ya afya iliyozidiwa mara moja ulipozuka ugonjwa huo, imepungua.

“Mtindo huu umeruhusu nchi nyingi kurejea katika maishani ya kawaida tulivyoyajua kabla ya COVID-19”, ameongeza Ghebreyesus.

Wauguzi wakifanya kazi katika kliniki ya chanjo ya Uviko-19 huko Rofunta, Sierra Leone, mnamo Desemba 2022. Picha | WHO/Michael Duff.

Tujifunze kwa makosa yetu

Ghebreyesus amesema katika kiwango kingine, ilikuwa wakati wa kutafakari kwa kina, huku ugonjwa huo ikiendelea kuacha makovu makubwa na ya muda mrefu kwenye ulimwengu wetu.

“Makovu haya lazima yawe ukumbusho wa kudumu wa uwezekano wa virusi vipya kuibuka, na matokeo mabaya kujitokeza”, amesema.

Makosa mengi yalifanyika, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uratibu, usawa na mshikamano, ambayo ilimaanisha kuwa zana na teknolojia zilizopo hazikutumiwa vyema kukabiliana na virusi.

“Lazima tujitahidi sisi wenyewe na watoto na wajukuu wetu, ili kwamba tusifanye makosa hayo tena,” amesema na kuongeza kuwa,

“Uzoefu huu lazima utubadilishe sote kuwa bora zaidi. Ni lazima utufanye tuazimie zaidi kutimiza maono ambayo mataifa yalikuwa nayo wakati yalipoanzisha WHO mwaka wa 1948, ambayo ni kuwa na kiwango cha juu zaidi cha afya kwa watu wote.”


Zinazohusiana:


WHO yatoa mapendekezo

Kufuatia taarifa hiyo yenye kuleta matumaini, WHO imetoa mapendekezo kwa mataifa yote ili kuhakikisha usalama wa wananchi wao kwani ugonjwa huo bado ni hatari

“Bado Uviko-19 inaua na bado inabadilika. Hatari inabaki katika lahaja mpya zinazoibuka ambazo husababisha kuongezeka kwa wagonjwa na vifo.” amesema Ghebreyesus.

Mapendekezo hayoyaliyotolewa na WHO ni pamoja na kuendeleza jitihada za kulinda afya za wasafiri hususani safari za kimataifa, kuendelea kuunga mkono tafiti mbalimbali ili kuboresha chanjo pamoja na kuongeza jitihada za kitabibu za kupambana na Uviko-19.

Kufuatia taarifa hiyo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’ameipongeza Serikali, watoa huduma za afya, wananchi pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo nchini Tanzania.


Tangu kuripotiwa mgonjwa wa kwanza wa Uviko 19 mwaka 2020 mpaka Mei 3, 2023 Tanzania imeripoti jumla ya wagonjwa 42,973 na vifo 846.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV