WHO yaidhinisha dawa mpya kupunguza makali virusi vya Uviko-19

September 25, 2021 6:23 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni dawa ya Regeneron ambayo huwasaidia ambao hawana kinga ya kutosha.
  • Wanapewa wagonjwa wenye Uviko-19 waliohatarini kulazwa hospitali.

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limeidhinisha matumizi ya dawa ya Regeneron kwa ajili ya kutibu watu wenye dalili kali za ugonjwa wa Corona (Uviko-19) na hawana kinga ya kutosha mwilini.

Dawa hiyo ambayo ni mchanganyiko wa dawa aina ya Casirivimab na Imdevimab inapendekezwa kutumika kwa wagonjwa ambao si wagonjwa mahututi lakini wako katika hatari ya kuweza kulazwa hospitalini kutokana na Uviko-19.

Hatua ya WHO imetangazwa Septemba 25, 2021 mjini Geneva, Uswisi na Dk  Janet Diaz kutoka Idara ya utabibu huku akisema akitaka gharama ya Regeneron ipunguzwe sambamba na usambazaji wake uwe sawia.

“Hii ni hatua kubwa sana,” amesema Dk Diaz akiongeza “ni pendekezo letu la kwanza la tiba kwa wagonjwa wenye dalili za kati au zisizo kali za Uviko-19 kwa sababu inapunguza uhitaji wa mgonjwa kulazwa iwapo huko kwenye hatari zaidi.”

Amesema matumizi ya dawa hiyo yatasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolazwa na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa WHO, hadi kufikia Septemba 24, kulikuwa na maambukizi milioni 240.5 ya Uviko-19 duniani huku vifo vilivyoripotiwa ni milioni 4.7.

Tiba hiyo ya kuongeza kinga ilipatiwa ruhusa ya matumizi ya dharura nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana baada ya kutumiwa kumtibu aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Donald Trump baada ya kulazwa hospitali alipougua Uviko-19.

Uingereza imeshaidhinisha matumizi ya Regeneron huku Muungano wa Ulaya (EU) bado unaifanyia tathmini.

Hatua ya WHO kuidhinisha dawa hiyo inazingatia matokeo kutoka utafiti uliofanyika nchini Uingereza kwa wagonjwa 9,000 waliotumia dawa hiyo na kudhihirisha kuwa inapunguza vifo kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitali na ambao kinga zao za mwili zilishindwa kukabiliana na virusi.

Dawa hiyo imekuwepo sokoni kwa miongo kadhaa kutibu magonjwa mengine kama vile saratani na msingi wake inatoa kingamwili vinavyofanana na vile vinavyozalishwa na mwili ili kupambana na maambukizi.

Kampuni ya Roche ya Uswisi imekuwa inatengeneza dawa hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya Regeneron inayomiliki hataza ya dawa hiyo.

Dkt. Diaz amesihi kampuni ya Regeneron kupunguza bei na iangalie uwezekano wa usambazaji kwa uwiano duniani kote.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV