Majaribio ya dawa kwa wagonjwa mahututi wa Uviko-19 yaanza

August 12, 2021 12:21 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • WHO itaanza majaribio ya dawa aina tatu ikiwemo ya ‘Artesunate’.
  • Dawa hizo zitatumiwa na wagonjwa mahututi wa Uviko-19.

Dar es salaam. Wakati dunia ikiendelea na mapambano dhidi ya Uviko-19, Shirika la Afya la Duniani (WHO), limetangaza kuwa litaanza majaribio ya dawa aina tatu kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa walio mahututi kutokana na ugonjwa huo.

Majaribio hayo yanatoa matumaini ya kupatikana kwa dawa ya ugonjwa huo hapo baadaye, licha ya kuwa watu wanapatiwa chanjo ili kuwakinga na maambukizi. 

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk Tedrosa Adhanom Ghebreyesus amesema kupitia mpango wa mshikamano wa majaribio ya dawa za kutibu Uviko-19 uliopewa jina la ‘Solidarity Plus’ watafanya majaribio ya dawa aina tatu katika nchi 52. 

Dawa hizo zitakazo fanyiwa majaribio ni ‘Artesunate’, ‘Amatinib’ na ‘Infliximab’ ambazo zilichaguliwa na jopo huru la wataalamu waliokuwa wanaangalia namna ya kusaidia kupunguza vifo wagonjwa wa Uviko-19 walio hospitali. 

“Kupata tiba bora na inayoweza kupatikana kwa wagonjwa wa Uviko-19 bado ni hitaji muhimu na WHO inajivunia kuongoza juhudi hii ya ulimwengu,” amesema Dk Tedros katika mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika Agosti 11, mjini Geneva, Uswisi.

Dawa hizo ambazo zimetolewa bure kwa ajili ya majaribio na wazalishaji wake si mpya kwani zimekuwa zikitumika katika kutibu magonjwa mengine. 

Artesunate inatumika kutibu malaria kali, Imatinib inatumika kutibu baadhi ya saratani, na Infliximab inatumika kwenye magonjwa kadhaa ya mfumo wa kinga pamoja na ugonjwa wa damu.  

Kampuni zilizotoa dawa hizo kwa ajili ya majaribio ni Ipca, Novartis pamoja na Johnson&Johnson. 


Mwanasayansi wa maabara akifanya utafiti katika kituo cha ushirikiano cha utafiti cha shirika la Afya la umoja wa mataifa nchini Thailand| WHO/Ploy Phutpheng.

 Solidarity Plus ni nini?

Jukwaa la majaribio, Solidarity PLUS ni jukwaa ambalo linawakilisha ushirikiano mkubwa zaidi ulimwenguni kati ya nchi wanachama wa WHO na linahusisha maelfu ya watafiti katika hospitali zaidi ya 600 katika nchi 52.

Kupitia jukwaa hilo watafiti kote ulimwenguni wana nafasi ya kutumia utaalamu wao na rasilimali kuchangia utafiti wa ugonjwa wa Uviko-19. 

Uwepo wa jukwaa hili unaruhusu majaribio ya kutathmini matibabu anuwai kwa wakati mmoja kwa kutumia itifaki moja, kujumuisha maelfu ya wagonjwa, kutoa makadirio thabiti juu ya athari ambayo dawa inaweza kuwa nayo juu ya vifo na pia hata athari za wastani. 

Hapo awali, dawa aina nne za ‘Remdesivir’, ‘Hydroxychloroquine’, ‘Lopinavir’ na ‘Interferen’ zinazotumika kuwapa ahueni wagonjwa mahututi wa Uviko-19 zilifanyiwa majaribio na jukwaa hilo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV