Uviko-19 kusababisha uhaba wa mabomba ya sindano?

November 22, 2021 7:37 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni (WHO) limesema juhudi za kuongeza uzalishaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona ziende sambamba na uzalishaji wa mabomba ya sindano yanayotumika kutoa chanjo hizo la sivyo kunaweza kuweko na uhaba mkubwa wa mabomba ya sindano yanayohitajika kwa ajili ya kampeni za chanjo za kawaida.

Mshauri mwandamizi wa WHO kuhusu upataji wa dawa na vifaa vya matibabu Lisa Hedman amesema kwa kuzingatia kuwa takribani watu bilioni 7 duniani kote wanahitaji dozi mbili za chanjo za Uviko-19 kati ya sasa na mwaka 2023 na kwamba kunaweza kuwapo na uhaba wa mabomba bilioni moja ya sindano.

Headman amesema kizazi kizima cha watoto kinaweza kukosa chanjo za kawaida iwapo wazalishajiwa mabomba ya sindano hatawakuwa na mpango mahsusi wa kutengeneza mabomba ya sindano ya kutumia mara moja na kutupa. 

“Unapofikiria kuhusu kiwango kikubwa cha sindano zinazotumika kwenye chanjo dhidi ya janga la Corona, hili ni jambo ambalo hupaswi kulitekeleza kwa mkato au kuweka upungufu wowote kwa ajili ya usalama wa wagonjwa na wahudumu wa afya,” amesema Headman.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV