Waziri Mkuu:Anzisheni majukwaa ya kiuchumi

December 30, 2022 11:49 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Majukwaa hayo yataongeza uwekezaji na kukuza soko la nje.
  • Yatafungua fursa za kiuchumi na kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kuanzisha majukwaa ya kiuchumi yatakayowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo ili kuvutia wawekezaji nchini.

Majaliwa aliyekuwa akizungumza na watumishi wa ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Pretoria, Afrika Kusini leo Disemba 30, 2022 amewataka viongozi na watumishi hao waendelee kufanya tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kupata kutokana na ushirikiano wa kidiplomasia kwenye nchi walizopo ili kuongeza uwekezaji nchini.

“Muwasihi wafanyabiashara na wawekezaji waje kuwekeza Tanzania na washirikiane na Watanzania kufungua makampuni, hii itatusaidia Watanzania kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha biashara,” amesema Majaliwa.


Soma zaidi


Amesema watumishi wa balozi za Tanzania hawana budi kuandaa makubaliano baina ya Tanzania na nchi walizoko ambayo yataonesha nini kinatakiwa nchini na ambacho kinapatikana kwa wingi nyumbani Tanzania.

“Hapa kwenu, ubalozi unapaswa kutengeneza makubaliano maalum ya kibiashara miongoni mwa nchi hizi mbili na kubainisha aina ya bidhaa ambazo zinapatikana Tanzania kwa wingi na zinahitajika Afrika Kusini,” amesisitiza Majaliwa.

Sambamba na hayo Majaliwa amewataka watumishi hao kuhamasisha watalii kutoka nchini humo kwa kubainisha vivituo vya utalii vilivyoko Tanzania ambavyo nchi hiyo haina huku akitolea mfano Mlima Kilimanjaro.

Awali, akitoa taarifa ya kiutendaji ya ubalozi huo, Kaimu Balozi Peter Shija alisema Tanzania inaweza kunufaika zaidi na fursa za biashara zilizopo nchini humo kwa kuuza mazao kama, mchele, maharage, korosho na mazao ya matunda.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV