Diaspora watakiwa ‘kuvaa ubalozi’ fursa Tanzania

October 29, 2022 6:19 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Waziri Mkuu awataka kushawishi na kuvutia uwekezaji nchini Tanzania.
  • Awataka kujenga taswira nzuri ya Tanzania huko waliko.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wanaoishi ughaibuni kuwa mabalozi wazuri kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi wanazoishi ili kujenga taswira nzuri ya Tanzania huko waliko.

Majaliwa aliyekuwa akizungumza na Watanzania waishio Jamhuri ya Korea jana (Oktoba 28, 2022) pia amewataka Watanzania hao watumie fursa walizonazo kushawishi na kuvutia uwekezaji nchini Tanzania.

 “Tumieni ushawishi na fursa mlizonazo kuwavutia wawekezaji na siku zote semeni mazuri na fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania bila kusahau kuwasemea vizuri viongozi wakuu hasa dhamira nzuri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuliletea maendeleo Taifa,” amesema Rais Samia. 

Majaliwa amewataka wajenge utamaduni wa  wa kutumia lugha ya Kiswahili kama fursa ya kiuchumi kwani nchi nyingi zinahitaji walimu, waandishi, watangazaji na wakalimani wa lugha hiyo ya Taifa.

Amewahakikishia kuwa Tanzania ipo salama na Rais Samia anafanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba maisha ya Watanzania  yanaimarika kwa kuendelea kusogeza karibu huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, umeme na elimu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Korea John Bakunda ameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuendelea kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na mataifa mbalimbali duniani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV