Mabalozi wapewa kibarua kuvutia wawekezaji, kutafuta masoko ya bidhaa

January 17, 2022 2:19 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 17, 2022 jijini Dodoma amekutana na mabalozi:  Balozi Profesa Adelardus Kilangi anayeenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil, Balozi Said Juma Mshana (DR-Congo), Balozi Alex Gabriel Kalua (Israel), Balozi Said Shaib Mussa (Kuwait) na Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta anayeenda Urusi. Picha| Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Ni wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
  • Watakiwa pia kuutangaza utalii na kuwasaidia Watanzania waishio nje ya nchi.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa kuhamasisha uwekezaji, kuimarisha biashara pamoja na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini katika maeneo yao ya uwakilishi.

Majaliwa amewasisitiza mabalozi hao kuhakikisha wanalinda taswira ya Tanzania katika nchi za uwakilishi sambamba na kujielekeza katika kuvutia watalii na kuwasaidia wafanyabiashara wa Kitanzania kufanya biashara nje.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Januari 17, 2022 jijini Dodoma alipokutana na mabalozi:  Balozi Profesa Adelardus Kilangi anayeenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil, Balozi Said Juma Mshana (DR-Congo), Balozi Alex Gabriel Kalua (Israel), Balozi Said Shaib Mussa (Kuwait) na Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta anayeenda Urusi.

Aidha, amewataka mabalozi hao wahakikishe wanakwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa balozi kwa kubana matumizi hususani katika mambo yasiyokuwa ya lazima. 

“Pia mkaimarishe mahusiano kati yenu na maafisa wa ubalozi,” amesema Majaliwa.

Mabalozi hao wametakiwa wakutane na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) na wawasaidie kuimarisha Jumuiya zao kwa kuwa na uongozi imara. 

“Waunganisheni ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na kwenye shughuli za kijamii mnazozifanya huko,” amesema Majaliwa na kubainisha kuwa,

“Naamini mkitumia ushawishi wenu katika kukitangaza Kiswahili kinaweza kuwa chanzo cha ajira kwa Watanzania nje hususan kwa walimu wa fani hiyo sambamba na kuitangaza nchi yetu.”

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake, Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Balozi Kilangi ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa kukutana nao na ameahidi kwamba hawatamuangusha Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake na kwamba watahakikisha wanakwenda kutekeleza maelekezo yote kwa manufaa ya Taifa.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV