Majaliwa: Hatutawatupa wawekezaji

November 29, 2022 6:47 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema Serikali itaendelea kufanya nao kazi kwa karibu.
  • Uwekezaji unasaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya nchi.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji ili kuhakikisha uwekezaji wao haukwami bali unakua na kuleta tija kwa Tanzania.

Waziri Maliwa ameyasema hayo Novemba 28, 2022  alipotembelea na kuweka jiwe la msingi kwenye  kiwanda cha  kutengeneza mabati cha Lodhia kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza kwenye kiwanda hicho Majaliwa amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wawekezaji nchini wanapata faida. 

“Tunathamini uwekezaji huu, tunaheshimu uwekezaji huu na tutakuunga mkono kwenye uwekezaji,” amesema Majaliwa. 

Amesema Serikali inatambua mchango wa wawekezaji katika kuchangia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, mawasiliano na hata ajira.

“Upanuzi wa kiwanda hiki ni kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada zake za kuendelea kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa Watanzania,” amesema Majaliwa.


Soma zaidi


Uwepo wa wawekezaji hao kwenye sekta mbalimbali  ikiwemo viwanda utasaidia nchi kuwa  na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa ndani ya nchi badala ya kuagiza kutoka nje pekee. 

“Leo hii hatuna haja sana ya kuagiza nondo Ulaya au Asia, nyingi zinapatikana hapa nchini ikiwemo kwenye kiwanda hiki cha Lodhia”

Aidha Waziri Mkuu amewataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuhakikisha malengo ya muwekezaji yanatimia. 

“Endeleni kufanya kazi vizuri kwenye kampuni hii, ninyi ni mabalozi wetu wazuri,” amesisitiza Majaliwa.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.