Ujenzi ghala la mafuta kupunguza bei ya petroli?

January 20, 2023 5:49 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kupata wawekezaji watakaojenga ghala kuu la kupokelea mafuta kwa pamoja.
  • Itawezesha Tanzania kuwa na uhakika zaidi wa upatikanaji wa mafuta.

Dar es Salaam. Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kupata wawekezaji watakaojenga ghala kuu la kupokelea mafuta kwa pamoja ili kuiwezesha Tanzania kuwa na uhakika zaidi wa upatikanaji wa mafuta.

Makamba ameyasema hayo Januari 19, 2023, wakati Wizara ya Nishati ikitoa taarifa ya mwenendo wa upatikanaji wa mafuta nchini kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

Amesema kuwa, uwepo wa ghala hilo utawezesha shehena kubwa za mafuta kupakuliwa kwa haraka na hivyo kupunguza gharama za uagizaji, ucheleweshaji wa meli na kuendelea kuleta unafuu wa bei za bidhaa za mafuta nchini.

“Serikali imeanza kutumia ghala la TIPER kwa ajili ya kupokea mafuta ya dizeli yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza muda wa kupokea mafuta hayo kutoka katika meli,” amesema Makamba.

Ameeleza kuwa, Serikali itajenga pia gati kubwa la kupokea mafuta ya petroli na kuboresha gati kubwa la kupokea mafuta ya dizeli.

Gati hizo zitaakisi mahitaji ya sasa na miaka ya baadaye ikiwemo kujenga gati kubwa lenye mabomba ya kupakua mafuta na kuwezesha kupokea meli kubwa zenye uwezo wa kubeba tani 100,000 za petroli, tani 200,000 za dizeli na tani  milioni 40 za gesi ya mitungi (LPG).

Aidha, amesema Serikali itaendelea kufuatilia mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji ili kuweza kuchukua hatua stahiki zitakazopunguza makali ya bei kwa wananchi na katika uchumi wa nchi.


Soma zaidi:


Kwa mujibu wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura),  Tanzania Bara ina ghala 22 za kupokelea mafuta zilizopo katika bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, zenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo milioni 1.3.

 Ghala hizo hupokea bidhaa za petroli kutoka melini. Aidha, kuna ghala 29 nchi kavu, zenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 75,625. 

“Hata hivyo, ghala hizo, nyingi hazifanyi kazi. Pia, Kampuni ya Bomba la Mafuta la TAZAMA inapokea mafuta ghafi kupitia boya (SBM) na kuhifadhi bidhaa hizo kwenye ghala lake lenye mita za ujazo 232,000,” imeeleza Ewura katika tovuti yake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dunstan Kitandula ameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali zinazochuliwa katika shughuli za upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na unafuu wa bei za bidhaa za mafuta katika soko la ndani.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya kuhifadhi mafuta ya TIPER pamoja na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV