Bei ya Petroli, dizeli yapaa Tanzania

February 5, 2025 10:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya rejareja ya petroli yafikia ShSh 2,820 na dizeli ShSh2,703.
  • Yapaa kwa mara kwanza baada ya kushuka kwa miezi mitano mfululizo.

Dar es Salaam. Watumiaji wa mafuta ya petroli, dizeli nchini Tanzania wanauanza mwezi Februari kwa maumivu ya  kupaa kwa bei ya nishati hizo baada ya kushuka kwa kipindi cha miezi mitano mfululizo tangu Agosti mwaka 2024.

Kwa kipindi cha miezi mitano iliyopita bei ya mafuta ya petroli na dizeli imekuwa ikishuka kwa wastani wa Sh100 hadi Januari mwaka 2025 ambapo nishati hizo ziliuzwa kwa Sh2,793 na Sh2,644 kwa kila lita mtawalia.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (Ewura) leo Februari 5, 2025 inaeleza kuwa bei ya rejareja ya petroli iliyoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam imepaa kwa Sh27  na dizeli kwa Sh39 kwa lita moja. 

Kwa bei hizo mpya bei ya rejareja ya petroli inayopitia bandari ya Dar es Salaam itakuwa Sh 2,820 kutoka Sh2,793 iliyorekodiwa Januari na dizeli itauzwa kwa Sh2,703 kutoka Sh2,644  iliyotumika katika mwezi wa kwanza wa mwaka 2025.

Mafuta ya taa pia yamepanda kwa Sh34 kwa lita  na kuuzwa kwa 2,710 kwa mafuta yanaoingizwa kupiti bandari ya Dar es Salaam 

Kwa mujibu wa Ewura, ongezeko hilo la bei huenda limechangiwa na kuongezeka kwa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) kwa asilimia 4.77.

“Gharama za mafuta (FOB) na gharama za uagizaji (Premiums) zinalipiwa kwa kutumia fedha za kigeni ikiwemo Dola ya Marekani. Kwa bei za mwezi Februari 2025, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umeongezeka kwa asilimia 4.77,” imesema taarifa ya Ewura.

Maumivu hadi mikoani

Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ndiyo inayonunua mafuta hayao kwa bei ya juu zaidi mwezi Februari kulinganisha mikoa mingine nchini ambapo lita moja ya Petroli inauzwa kwa Sh3,058 huku dizeli ikuzwa kwa Sh2,941.

Januari mwaka huu, wilaya hiyo iliuziwa lita moja ya Petroli kwa Sh3,031 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh2,882.

Wakati wakazi wa wilaya hiyo mkoani Kagera wakiugulia maumivu ya kununua mafuta hayo kwa bei ya juu, Ewura inabainisha kuwa mkoawa Dar es Salaam ndiyo unaonunua mafuta hayo kwa bei ndogo zaidi kulinganisha mikoa mingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks