Majaliwa: Mabasi ya mikoani, madereva wawili

March 14, 2023 1:12 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link


  • Asema hiyo itasaidia kuwaondolea uchovu wakiwa barabarani
  • Ni njia mojawapo ya kupunguza ajali za barabarani.

Mwanza. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi nchini na wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria kwenda mikoani kuhakikisha kunakuwepo na madereva wawili watakaosaidiana kuendesha mabasi ili kupunguza ajali za barabarani. 

Majaliwa aliyekuwa akizungumza kwenye uzinduzi ya wiki nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika jijini Mwanza, leo Marchi 14, ametaja safari ndefu za mabasi yaendayo mikoani ndiyo zinaongoza kuwa na ajali nyingi huku sababu ikitajwa kuwa ni uchovu wa madereva wawapo barabarani.

Waziri Majaliwa amesema takwimu za Jeshi la Polisi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuanzia 2020 hadi 2022 inabainisha jumla ya ajali 5,132 zilitokea nchini huku vifo vya abiria vikiongoza kwa kuwa na takwimu kubwa.

Amesema katika kipindi hicho, jumla ya vifo 1,582 vya abiria vilitokea  na na wengine 4,372 wakijeruhiwa.

Madhara mengine yaliyotokea ni kwa watembea kwa miguu ambapo vifo 959 vilitokea katika kipindi hicho na majeruhi wakiwa 650 na waendesha pikipiki takwimu zinaonyesha kuwa vifo vilikuwa 797 na majeruhi wakiwa 725.

“Katika kipindi hicho cha miaka mitatu ajali hizo zilisababisha vifo vya watu 4,060 na majeruhi 6,017,” amesema Majaliwa.

Amesema kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha anadhibiti ajali za barabarani kwa kuwa zimekuwa chanzo cha maumivu kwa wananchi kupoteza mali na nguvukazi katika sekta mbalimbali za umma na binafsi.

Sababu nyingine inayotajwa kuchangia ajali za barabarani ni madereva kuendesha vyombo cha moto wakiwa wamelewa, baadhi ya madereva kutokuwa na mafunzo, kubeba abiria kupita kiasi.


Zinazohusiana:


Fanyeni haya

Waziri Mkuu ametoa maagizo 12 kwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ikiwemo mapendekezo ya mchakato wa kupata sheria mpya ya usalama barabarani yafanyike haraka ili kupunguza ajali hizo.

Pia kuhakikisha mfumo wa kuweka alama kwenye maeneo hatarishi unazingatiwa.

Waziri Mkuu pia ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kukamilisha kufunga vifaa vya kielektroniki vitakavyosaidia kulinda maadili kwa madereva.

Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura amesema katika siku za hivi karibuni wamebaini chanzo kingine cha ajali kuwa ni mfumo mbovu wa upatikanaji wa madereva.

“Pia tumebaini kuwepo kwa baadhi ya vyuo vya udereva wanakosa sifa na weledi na kutumika kama madaraja ya vyeti feki na wasajili wa madereva kutoa leseni bila kufuata taratibu,” amesema IGP Wambura.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Jumanne Sagini amesema tayari wameanza kufanyia maagizo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha kila basi linafungwa kidhibiti mwendo ili kuhakikisha linafuatiliwa basi hilo popote linakokwenda.

“Tayari kwa baadhi ya mabasi yameanza kufungwa vidhibiti mwendo hivyo  lakini pia baraza limeendelea na mikakati ya kudhibiti madereva walevi, magari mabovu na magari yasiyokuwa na bima,” amesema Sagini.

Baraza limeanza kufanyia kazi suala la ukaguzi wa vyombo vya moto kupitia vifaa maalum kwa kushirikisha taasisi binafsi.

Amesema pia wameanza kutumia teknolojia za kisasa katika kutekeleza sheria za usalama barabarani vikiwemo vipimo vya ulevi kwa madereva.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV