Youtube yawaongezea nguvu wanamitindo duniani

September 6, 2019 11:13 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongeza kipengele kipya kwa ajili ya mitindo baada ya kubaini kuwa ina wafuasi wengi. 
  • Kitasaidia kuongeza mapato na ukuaji wa tasnia hiyo duniani.

Mtandao wa Youtube ambao uko chini ya kampuni ya Google umeamua kuipa kipaumbele tasnia ya mitindo baada ya kuanzisha kipengele kimpya kwa ajili shughuli hizo.

Mabadiliko hayo yamefanyika kufuatia tafiti iliyofanywa na mtandao huo na kubaini kuwa watumiaji wengi katika mtandao wana chaneli zenye maudhui hasa ya yanayohusu mitindo, mavazi na urembo. 

Kipengele hicho kinadhihirisha wazi kuwa Youtube imekusudia kuboresha huduma zake na kukidhi mahitaji ya watu wanaotembelea mtandao huo kila siku. 

Kwa mujibu wa Youtube, maudhui ya mitindo na usanifu wa mavaziyameongezeka zaidi ya mara sita kati ya mwaka 2014 na 2018, jambo linatoa fursa kwao kuweka msisitizo katika tasnia hiyo inayoajiri watu wengi duniani.


Zinazohusiana:


Mabadiko hayo yamefanyika wiki hii kwa Youtube kuonyesha shughuli mbalimbali za mitindo ikiwemo matamasha ya mitindo na mavazi yanayofanyika maeneo mbalimbali duniani ili kuwarahisishia watu kuyaona wakiwa popote duniani. 

Youtube inaamini kuwa kipengele hicho kitachagiza ukuaji wa tasnia ya fasheni duniani na kuongeza mapato ya mtandao huo na watu waliowekeza katika shughuli hizo.

Youtube kutambua mchango wa wanamitido duniani. Picha| Mtandao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV