Wathibitishaji habari waiandikia waraka mzito YouTube kupinga upotoshaji mtandaoni

January 19, 2022 9:05 am · Wilson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wamtaka mkurugenzi wa YouTube kuchukua hatua katika kupambana na uzushi.
  • Wamtaka mkurugenzi kushughulikia sera za mtandao huo.
  • Waja na mapendekezo manne ya kufanyia kazi ili kuleta suluhu.

Dar es Salaam. Mtandao wa wathibitishaji habari duniani umemwamdikia barua ya wazi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya YouTube, Susan Wojcicki kuhusu madai ya kuendelea kuwepo kwa habari potofu katika jukwaa hilo linalochapisha maudhui kwa njia ya video.

Barua hiyo ya wazi imeanza kusambazwa  Januari 12,2022 na shirika la uthibitishaji habari la PesaCheck  kwa kushirikiana na kampuni ya  Code for Africa (CfA) ikihusisha mtandao washirika wengine 60 kutoka mataifa 80.

Barua hiyo inalenga kumshinikiza mkurugenzi huyo na YouTube kuchukua hatua ya kuunga mkono juhudi za kupambana na habari za uzushi ambazo baadhi yake zimekuwa zikisambazwa kupitia YouTube.

“Kile ambacho hatuoni ni juhudi nyingi za YouTube kutekeleza sera zinazoshughulikia tatizo. Badala yake, YouTube inaruhusu jukwaa lake kumilikiwa na watumiaji wasio waaminifu ili kuwadanganya na kuwaumiza wengine,” imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Miongoni mwa habari za uzushi ambazo zinaozitesa dunia kwa sasa ni zile zinazohusu janga la Corona (Uviko-19) ambapo zimezidisha madhara ya ugonjwa huo hasa katika sekta ya afya na uchumi.

Majukwaa ya mtandaoni ikiwemo YouTube imekuwa sehemu ambazo habari hizo husambazwa licha ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wamiliki wa mitandao ya kijamii kudhibiti habari hizo.

Mtandao wa YouTube umekuwa ukitumiwa na baadhi ya watu kupenyeza habari za uongo kwenye jamii. Picha|Mtandao.

Barua hiyo imedai kuwa kuna uzembe unaofanywa na YouTube juu ya maudhui yenye nia ovu hususani katika mataifa yasiyozungumza lugha ya Kiingereza na kulalamikia sera zake kwamba zipo lakini hazitiliwi maanani.

“Mifano ni mingi mno kuhesabu.  Video nyingi na idhaa hizo zimesalia mtandaoni leo, na zote ziliingia chini ya sera za YouTube, hasa katika nchi zisizozungumza Kiingereza na na zile za ukanda wa Kusini mwa dunia. 

“Tunafurahi kwamba kampuni imechukua hatua kujaribu kushughulikia tatizo hili hivi karibuni lakini kulingana na kile tunachoona kila siku kwenye jukwaa, tunafikiri kwamba jitihada hizi hazifanyi kazi wala YouTube haijatoa data yoyote ya ubora ili kuthibitisha ufanisi wao,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Mbali na hayo waraka huo wa wazi umetoa mapendekezo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kama suluhisho katika kupambana na habari za uzushi katika mtandao huo:

1, Kujitolea katika kuweka uwazi katika mtandao huo ili kuruhusu wathibitishaji binafsi kufanya uchunguzi bila vizuizi.

2. Kuondoa maudhui kwa ajili ya utii wa sheria. Lengo la YouTube linapaswa kutoa muktadha na kutoa mada, zinazowekwa wazi zaidi kwenye video au kama maudhui ya ziada ya video.

3. Kuchukua hatua kali dhidi ya wakosaji wa mara kwa mara ambao hutoa maudhui ambayo yanaripotiwa kila mara kama habari potovu na upotoshaji, hasa wale wanaopata mapato ya yaliyomo ndani na nje ya jukwaa.

4. Kuongeza juhudi za sasa na zijazo dhidi ya taarifa potofu na upotoshaji katika lugha tofauti na Kiingereza, na kutoa data ya nchi na lugha mahususi, pamoja na huduma za unukuzi zinazofanya kazi katika lugha yoyote.


Soma Zaidi:


Hatua zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii

Licha ya barua hiyo, mitandao ya kijamii imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na habari za uzushi mtandaoni.

YouTube  ina sera ya kukabiliana na maudhui ya upotoshaji ambapo hutumia  mashine maalumu ili kuondoa maudhui ambayo yanakiuka sera zake haraka iwezekanavyo.

Mtandao wa Instagram na Facebook, zilichukua hatua ya kuanza kufanya kazi na shirika la Marekani katika uthibitishaji habari ili kuweza kukagua na kubaini taarifa za uongo.

Washirika hao hutathmini taarifa za uongo kwa uhuru ili kusaidia kuzipata na kupunguza usambazaji wake.

Lakini pia mtandao wa Twitter huweka lebo mpya za maonyo katika machapisho ya watumiaji wake ambazo  zimeunganishwa na kurasa zilizoratibiwa za mtandao huo ili kubaini taarifa za uongo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV