WhatsApp kuendelea na sera yake mpya ya faragha yenye utata

February 20, 2021 8:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni sera ya faragha ambayo imeibua mjadala mpana duni kuhusu usiri wa taarifa za watumiaji wake.
  • Yasema itaanza kuwakumbusha watumiaji wake kuipitia na kukubali masasisho ya sera hiyo ili kuendelea kupata huduma za jukwaa hilo la mtandaoni.

Mtandao wa WhatsApp ambao unamilikiwa na kampuni ya Facebook Inc umesema utaendelea na mchakato kusasisha (update) sera yake mpya ya faragha yenye utata iliyoibua mjadala mpana duniani.

Wakati ikiendelea kusasisha sera hiyo, itawawezesha watumiaji wake kuisoma kwa muda wao huku ikitoa tangazo la taarifa za ziada kuhusu sera hiyo.

Mapema January mwaka huu, jukwaa hilo la mawasiliano ya ujumbe mfupi liliwatangazia watumiaji wake kuwa linaandaa sera mpya ya faragha ambayo kwa sehemu itashirikisha taarifa zao binafsi na mtandao wa Facebook na makundi mengine inayoyasimamia.

Tangazo hilo liliibua  mjadala mpana duniani huku baadhi ya watumiaji wakichukua maamuzi magumu ya kuhamia Telegram na Signal ili kulinda taarifa zao.



Kutokana na suala hilo, WhatsApp ilisogeza mbele uzinduzi wa sera hiyo hadi Mei mwaka huu badala ya tarehe ya awali ya mwezi Februari ili kutoa fursa ya kuwaelimisha watumiaji wake juu ya mabadiliko hayo mapya.

Hata hivyo, Februari 18 mwaka huu katika blogu yake, WhatsApp  imesema itaanza kuwakumbusha watumiaji wake kuipitia na kukubali masasisho ya sera hiyo ili kuendelea kupata huduma za jukwaa hilo la mtandaoni.

“Pia tumejumuisha taarifa zaidi kujaribu na kutatua malalamiko ambayo tunayasikiliza, imeeleza sehemu ya blogu hiyo.

WhatsApp itafanikiwa?

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV