WhatsApp yatimiza miaka 12, ikikosolewa kwa sera yake mpya

February 26, 2021 7:40 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Mtandao huo uliasisiwa mwaka 2009 na waliowahi kuwa wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Yahoo Inc, Jan Koum na Brian Acton na ilipofika February 2014 programu hiyo tumishi iliuzwa kwa Dola za Marekani 19.3 bilioni kwa mmliki wa Facebook, Mark Zuckerberg. Picha|Daniel Samson.


  • Mtandao huo ulianzishwa mwaka 2009 na mwaka 2014 ulinunuliwa na kampuni ya Facebook
  • Ni maarufu kwa kutuma meseji, kupiga simu za sauti na video kwa njia ya intaneti.
  • Licha ya mafanikio yake, inakoselewa kwa sera yake mpya ya faragha ambayo itaanza kutumiaka Mei 15 mwaka huu. 

Mtandao wa WhatsApp umetimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake huku ikitaja mafanikio mbalimbali ikiwemo kulifanya jukwaa hilo kuwa sehemu muhimu ya watu kuwasiliana duniani kwa meseji za mtandaoni..

Mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Facebook Inc ya Marekani umetangaza kusherekea siku yake ya kuzaliwa Februari 25, 2021 na kubainisha kuwa kwa sasa inasimamia zaidi simu bilioni 1 zinazopigwa katika mtandao huo kila siku. 

WhatsApp ilivua nanga rasmi Februari 2009 na awali ilisainifiwa kwa ajili ya kusambaza mawasiliano hasa yanayohusu hali (statuses) za watumiaji wake. Lakini baadaye ilijitanua zaidi na kuanza kutoa huduma ya meseji, ujumbe wa sauti na video. 

Kwa sasa, mtumiaji wa mtandao huo unawawezesha watumiaji wake kufanya malipo na kutuma stika za namna mbalimbali ili kurahisha maisha hawa kwa watumiaji wa intaneti.Kupitia ujumbe wake wa Twitter uliowekwa jana, WhatsApp imesema inapata watumiaji hai zaidi ya bilioni 2 kila mwezi ambao wanatuma meseji zaidi bilioni 100. 

Mtandao huo uliasisiwa mwaka 2009 na waliowahi kuwa wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Yahoo Inc, Jan Koum na Brian Acton na ilipofika February 2014 programu hiyo tumishi iliuzwa kwa Dola za Marekani 19.3 bilioni kwa mmliki wa Facebook, Mark Zuckerberg.

Katika kipindi cha miaka 12 tangu kuanzishwa kwake, WhatsApp pia inajivunia kuangiza sokoni programu tumishi ya biashara (WhatsApp Business App) iliyoanzishwa mwaka 2018 ambapo wafanyabiashara wanapata fursa ya kuonana na wateja na  kujua kwa undani mwenendo wa biashara siku kwa siku.

Hata hivyo, mafanikio ya miaka 12 ya WhatsApp huenda yakaingia doa kutokana na mjadala makali unaoendelea sasa mtandaoni kuhusu sera yake mpya ya faragha ambayo inatarjiwa kuanza kutumika Mei 15 mwaka huu.


Soma zaidi: 


Januari 2021, WhatsApp ilitangaza sera hiyo na kuwataka watumiaji wake wakubali masharti na vigezo vyake ili waendelee kuitumia, lakini ilipata upinzani mkali kutokana na baadhi ya vipengele vya sera hiyo kutokuwafurahisha watumiaji wake. 

Miongoni mwa mambo yanayopingwa katika sera hiyo mpya ni WhatsApp kubadilishana taarifa na data za watumiaji wake na Facebook, jambo ambalo limelalamikiwa na watu kuwa hakutakuwa na usiri wa taarifa za watumiaji. 

Hata hivyo, WhatsApp mara kadhaa imesema haina nia mbaya kuhusu taarifa za watumiaji wake na itahakikisha usiri unakuwepo na imeendelea  kushikilia msimamo wake kuwa watumiaji ambao hawatakubaliano na masharti hayo mapya, akaunti zao zitafungiwa itakapofika Mei 15.

Kutokana na mkanganyiko huo, baadhi ya watumiaji wake wameanza kutafuta mitandao mingine ikiwemo Telegram na Signal ili kujiweka salama. 

Wakati WhatsApp ikitimiza miaka 12, una lipi la kukumbuka ambalo huenda limechangia katika mafanikio ya shughuli zako?

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV