WhatsApp kuzima mawasiliano kwa wasiokubaliana na sera mpya

February 23, 2021 6:31 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni sera mpya ya faragha ambayo imepokewa kwa hisia tofauti.
  • Zoezi hilo litafanyika ifikapo Mei 15 mwaka huu.

Watumiaji wa WhatsApp ambao hawatakubali kanuni na masharti mapya ya mtandao huo ifikapo Mei 15 mwaka huu hawataweza kupokea wala kutuma ujumbe katika mtandao huo mpaka wakubaliane utaratibu huo.

Kwa ambao hawatakubaliana na matakwa hayo, akaunti zao zitawekwa katika orodha maalum ya akaunti zisizofanya kazi (inactive) na akaunti hizo zisipohuishwa zinaweza kufutwa baada ya siku 120.

Mapema January mwaka huu, jukwaa hilo la mawasiliano ya ujumbe mfupi liliwatangazia watumiaji wake kuwa linaanda sera mpya ya faragha ambayo kwa sehemu itashirikisha taarifa zao binafsi na mtandao wa Facebook na makundi mengine inayoyasimamia.

Tangazo hilo liliibua  mjadala mpana duniani huku baadhi ya watumiaji wakiamia Telegram na Signal ili kulinda taarifa zao.


Soma zaidi:


Kutokana na suala hilo, WhatsApp ilisogeza mbele uzinduzi wa sera hiyo hadi Mei badala ya tarehe ya awali ya Februari ili kutoa fursa ya kuwaelimisha watumiaji wake juu ya mabadiliko hayo mapya.

Duru za kimataifa zinaeleza kuwa WhatsApp itaendelea na mpango wake licha ya maoni tofauti kutoka kwa watumiaji wake.

Uongozi wa mtandao huo umeeleza mara kadhaa kuwa sera hiyo mpya ina nia njema wala haikusudii kuweka wazi taarifa watumiaji wake.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Dk. Ndumbaro: Suala la utawala bora watu wanaliangalia kwa mtazamo finyu.

Dk. Ndumbaro: Suala la utawala bora watu wanaliangalia kwa mtazamo finyu.

Nukta TV

Kama huingizi angalau Sh750,000 kwa mwezi, hii inakuhusu

Kama huingizi angalau Sh750,000 kwa mwezi, hii inakuhusu

Nukta TV

Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Nukta TV