Wasafi TV yafungiwa miezi sita

January 5, 2021 12:50 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada yanakiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za mwaka 2018.
  • Yadaiwa kutangaza maudhui yasiyofaa yaliyomuonyesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake jukwaani.
  • Yatakiwa pia kuomba radhi kwa umma wa Watanzania. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha televisheni cha Wasafi TV kwa muda wa miezi sita kwa kutangaza maudhui yasiyofaa yaliyomuonyesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake jukwaani.

TCRA imesema maudhui hayo yanakiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za mwaka 2018.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, Mnamo Januari 1, 2021 majira ya 2:00 hadi saa 5:00 usiku kupitia kipindi cha “Tumewasha Live Concert” Wasafi Tv ilirusha maudhui jongefu yaliyokuwa yakimuonyesha msanii anayejulikana kwa jila la Gift Stanford Joshua Mwakyusa au “Gigy Money” akicheza katika jukwaa katika mitindo iliyokua ikionyesha utupu wa mwili wake. 

Kutokana na kosa hilo, TCRA imesitisha utoaji wa huduma ya matangazo za Wasafi TV kwa muda wa miezi sita kuanzia kesho Januari 6 hadi Julai 6, 2021. 

Aidha, TCRA imeitaka runinga hiyo kuahirisha matangazo na kutumia muda uliobaki leo kuomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kukiuka kanuni za utangazaji. 

“Iwapo Wasafi TV itashindwa, itakataa au itakaidi uamuzi huu, hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi ya Wasafi TV,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa TCRA, Johanes Kalungule iliyotolewa leo Januari 5, 2021.


Zinazohusiana:


Wasafi TV iliyopata leseni ya kitaifa ya utoaji wa huduma ya maudhui ya kulipia kwa njia ya televisheni Agosti 2019 imekua kiungo muhimu kwa wasanii wa Tanzania kuonyesha kazi zao za muziki ambazo zimekuwa zikiwapatia kipato. 

Hii itakuwa mara ya pili kwa chombo cha habari kinachomilikiwa na kampuni ya Wasafi Media kufungiwa kwa kukiuka kanuni za utangazaji. Septemba 11, 2020, TCRA iliifungia redio ya Wasafi FM kwa muda wa siku saba baada ya kutumia lugha za matusi kwenye vipindi vyake vya “The Switch” na “Mashamsham”.

Hata wakati, Wasafi TV ikifungiwa, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) imemfungia Gigy Money kujihusisha na kazi za sanaa ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi sita, na kumuamuru kulipa faini Sh1 milioni. 

BASATA imesema mwanamuziki huyo alivua gauni jukwaani na kubaki na vazi lililoonyesha maungo yake ya mwili wakati akitumbuiza jukwani jijini Dodoma Januari 1, 2021.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV