Jinsi ya kugundua kama Whatsapp yako imedukuliwa

April 27, 2024 2:10 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kukuta ujumbe mpya umetumwa, kusomwa au kufutwa na mtu usiyemfaahamu.
  • Ili kujilinda na udukuzi epuka kuunganisha simu yako na WiFi za bure ambazo huna uhakika nazo.

Dar es Salaam. Usalama mtandaoni ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa kwa upana kutokana na kuongezeka kwa wimbi la uvujishaji wa taarifa binafsi ikiwemo picha, video, sauti na soga katika mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa mitandao ambayo iko hatarini kutumiwa na wadukuzi kuvujisha taarifa binafsi ni Whatsapp inayomilikiwa na kampuni ya Meta.

Ndio! Hivi sasa si lazima uibiwe simu ndipo wadukuzi waweze kuiba taarifa zako. Mtandao wa Whatsapp pekee unatosha kuweka taarifa zako binafsi hatarini.

Matumizi ya mtandao huo yameshika kasi duniani kote ikiwemo Tanzania ambapo ripoti ya Takwimu za Mawasiliano ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) inautaja kushika nafasi ya nne kwa matumizi nchini.

Ripoti hiyo ya robo ya nne kwa mwaka 2023 inabainisha kuwa kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka 2023 mtandao huo ulitumia Jigabaiti 33.2 milioni nchini ikiashiria matumizi ya juu miongoni mwa wamiliki wa simu janja na vifaa vingine vinavyoweza kuunganishwa na mtandao.

Matumizi hayo yameongezeka kwa Jigabaiti 1 milioni ndani ya kipindi cha miezi mitatu ukilinganisha na Jigabaiti 32.2 milioni zilizorekodiwa katika robo ya tatu.


Soma zaidi:Tanzania kuunga mkono upatikanaji amani Somalia


 Utajuaje simu yako imedukuliwa?

Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya mtandao huo Mtaalamu binafsi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Zakia Mrisho amesema miongoni mwa dalili za kujua kuwa simu yako imedukuliwa ni pamoja na uwepo wa programu tumizi (apps) nyingi ambazo sio zako na hujawahi kuzipakua.

“Ili mtu adukue simu yako lazima awe na data muhimu kukuhusu ili kufanikisha hilo lazima a-install (kupakua)  ‘app’ apya ili kupata taarifa hizo, hivyo kuhakikisha kama ni salama ni vyema kuhakiki jina la app kupitia Google au kampuni uliyonununua simu,” amesema Zakia.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo dalili nyigine ni simu kuisha chaji ghafla na matumizi makubwa ya bando kuliko ilivyokuwa siku za nyuma, hiyo inaashiria kuwepo kwa ufanyaji mkubwa wa mfumo wa simu kupitia app ambazo wadukuzi wamezipakia.

Unaweza pia kugundua kuwa umedukuliwa ikiwa kila mara unakuta ujumbe mpya umetumwa, kusomwa au kufutwa wakati muda wote ulikuwa na simu yako karibu. Hii inaashiria kuwepo na mtu mwingine mwenye uwezo wa kutazama taarifa hizo.

“Wakati mwingine unakuta namba mpya ambazo hujazihifadhi zimehifadhiwa katika simu yako na kuunganishwa Whatsapp, labda hata zimetumiwa ujumbe fulani au umekuta akaunti yako yako imeunganishwa  na vifaa vingine vya mawasiliano ikiwemo ‘laptops’ (kompyuta mpakato) kupitia Whatsapp web,” ameongeza Zakia.

Ni vyema kutazama akaunti yako ya Whatsapp mara kwa ara ili kujua kama imeunganishwa na kifaa kingine cha mawasiliano.Picha|Adroid centre.

Jinsi unavyoweza kujilinda na udukuzi 

Ili uweze kuepuka au kujilinda na udukuzi Zakia anasema utakiwa kuhakiki app zote zilizopo katika simu yako ikiwa kuna unayoitilia mashaka ifute.

Pia acha tabia ya kubofya viunganishi vya mtandaoni unavyotumiwa WhatsApp pamoja na  kuchagua sehemu ya ‘charge only’ unapotumia ‘laptop’ kuchaji simu ili kuepuka kuhamishia taarifa zako katika kifaa hicho.

Enable Notifications OK No thanks