Wanafunzi vyuo vya kati Tanzania kupewa mikopo 2023-24

June 15, 2023 2:03 pm · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Fani za sayansi, afya, elimu pamoja na ufundi kupewa kipaumbele.
  • Kuanza kutekelezwa Julai 2023 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
  • Ni kufuatia mabadiliko sera ya elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imependekeza kuwapa mikopo wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati ambao  watakaosoma fani za kipaumbele kama vile sayansi, afya pamoja na elimu kuanzia Julai 2023.

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba aliyeukuwa akisoma hotuba ya Najeti Kuu ya Serikali bungeni jijini Dodoma amewaambia wabunge kuwa mapendekezo hayo ni kutokana na mabadiliko sera ya elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

“Serikali inalenga kutoa elimu ya amali kwa ngazi zote kuanzia shule za awali,  elimu ambayo inamwezesha kijana wa kitanzania kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa hili,” amesema  Dk. Nchemba.

Hata hivyo Waziri Nchemba ameongeza kuwa kuanzishwa kwa programu hiyo ya mikopo itawalenga wanafunzi waliochaguliwa na Serikali kusoma kwenye vyuo vya kati vya elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi elimu afya ufundi na elimu.


Soma zaidi;


Hatua hiyo itaanza kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza  watakao chaguliwa kujiunga katika vyuo kati kwa mwaka mpya wa fedha 2023/24

Aidha hatua hii inakuwa ni miongoni mwa mabadiliko ya mtaala katika sekta ya elimu yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inakusudia kukamilisha mabadiliko ya Sheria ya Elimu pamoja na kuanza utekelezaji wa mitaala mipya  kwa ngazi zote  kuanzia Julai 2023.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV