Mbinu zitakazosaidia walimu, wanafunzi kujikinga na Corona

July 5, 2021 6:12 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yaagiza shule, vyuo viwe na vifaa vya kunawa mikono.
  • Uvaaji barakoa na kuepuka mikusanyiko ya watu uzingatiwe.
  • Elimu zaidi ya kujikinga izidi kutolewa.

Mwanza. Wakati wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakianza masomo leo baada ya likizo ya mwezi Juni kumalizika, Serikali imetoa mwongozo utakaosaidia wanafunzi na walimu kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Mwongozo huo wa 16 utasaidia shule kuendelea kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kuwa na vifaa vya kunawa mikono, vitakasa mikono katika maeneo yao pamoja na kuhimiza uvaaji wa barakoa wakati wote.

Mwongozo huo pia umezielekeza shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi, uongozi uweke utaratibu wa wanafunzi hao kuingia kwa awamu ili kuepusha msongamano madarasani.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Abel Makubi katika taarifa yake iliyotolewa Juni 4, 2021 amesema  wanafunzi watakaobainika kuwa na dalili za kuumwa, wafanyiwe vipimo kabla ya kurudi shule.

“Wanafunzi watakaobainika kuwa na maambukizi wabaki nyumbani hadi hapo afya zao zitakapoimarika,” amesema Prof Makubi katika taarifa yake kuhusu mwongozo wa kujikinga na Corona shuleni, vyuoni na taasisi za elimu.

Wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Isebya katika ya Isebya, Wilaya ya Mbogwe. Picha| Gift Mijoe.

Pia wanafunzi watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Corona wakiwa shule au chuoni, uongozi wa shule utoe taarifa kwenye kituo cha huduma kilicho karibu ili kuwapatia matibabu wagonjwa.

Kwa upande wa wamiliki wa magari, Prof Makubi amesema abiria na wahudumu wote wahakikishe wanavaa barakoa na kutumia kitakasa mikono kabla ya kupanda na wakati wa kushuka  pamoja na kuvaa barakoa. Agizo hili ni kwa magari yote ya usafirishaji wa abiria na magari ya shule.

Katibu Mkuu huyo ameagiza kuhakikisha uongozi wa shule unazingatia kuwa watumishi wote na wanafunzi wanakaa kwa umbali usiopungua mita moja kati ya mtu na mtu.

“Walezi wa mabweni wapewe mafunzo na namna ya kubaini ishara na mbadiliko ya mwanafunzi pia wafanye ukaguzi mara kwa mara mabweni na afya za wanafunzi,” amesisitiza.

Wataalam wa afya ya jamii wametakiwa kuwafundisha walimu na wafanyakazi wa taasisi za elimu jinsi ya kujikinga na Corona na ikiwezekana mifumo ya Tehama itumike ili kuepusha wanafunzi kukutana.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV