Waliofariki ajali ya ndege Precision Air wafikia 19, Serikali yaagiza uchunguzi

November 7, 2022 4:10 am · admin
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mmoja wa wahanga wa ajali ya ndege ya Precision Air. Pichal Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Idadi ya watu wanaohisiwa kuwa ndani ya ndege yafikia 45 kutoka 43.
  • Uchunguzi kufanyika kubaini chanzo cha ajali.

Dar es salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema watu 19 wamepoteza maisha baada ya ndege ya Shirika la ndege la Precision Air kupata ajali katika Ziwa Victoria wakati ndege ikitua katika uwanja wa ndege wa Bukoba

Idadi hiyo ya watu 19 waliofariki inafanya watu waliohusiswa kuwa katika ndege hiyo kufikia 45. Awali Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Precision Air walisema watu 43 walikuwapo kwenye ndege hiyo.

Waziri Majaliwa amewaambia Watanzania mamlaka husika zinaendelea na uchuguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 19.

“Tunasikitika kwamba tumewapoteza ndugu zetu 19 baada ya zoezi la uokozi kukamilika kwa taarifa nilizonazo tunaamini mle ndani hajabaki mtu lakini uchunguzi unaendelea,” amesema Majaliwa.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Precision Air Patrick Mwanri ndege hiyo yenye namba PW 494 ilikuwa imetokea jijini Dar es Salaam ikiwa na watu 43 wakiwemo abiria 39, wahudumu wawili na marubani wawili.

Kutokana na kuwepo kwa mkanganyiko wa idadi halisi ya watu waliokuwepo ndani ya ndege, Majaliwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza suala hilo. Majaliwa amesema kwa sasa kinachoendelea ni zoezi la utambuzi wa miili ya watu waliopoteza maisha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV