Waliofariki ajali ya ndege Ziwa Victoria wanaagwa leo

November 7, 2022 6:41 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Zoezi laongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 

Dar es salaam. Miili ya watu 19 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea jana inaagwa hii leo katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albart Chalamila shughuli ya kuagwa kwa miili hiyo itaongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaaga miili hiyo itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Ndege hiyo yenye namba PW 494 ya kampuni ya Precision Air ilikuwa imetokea jijini Dar es Salaam ikiwa na watu 43 wakiwemo abiria 39, wahudumu wawili na marubani wawili ilianguka katika Ziwa Victoria umbali wa mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba.


Zinazohusiana

Waliofariki ajali ya ndege Precision Air wafikia 19, Serikali yaagiza uchunguzi


Taarifa iliyotolewa na Shirika la Ndege la Precision Air imefafanua kwamba waliookolewa katika ajali hiyo ni watu 24 na waliopoteza maisha ni 19 na kufanya idadi ya watu wanaohusishwa kuwa  ndani ya ndege kuwa 43

Awali kulikuwa na mkanganyiko wa idadi rasmi ya abiria waliokuwepo ndani ya ndege hiyo ambapo ilielezwa waliokolewa ni 26 na waliofariki ni 19 na kufanya jumla ya watu 45 tofauti na idadi iliyotajwa awali.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV