Wafuasi 34 wa Mfalme Zumaridi wapata dhamana

March 17, 2022 2:51 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya wakili wao kuwasilisha ombi mahakamani.
  • Walioachiwa mpaka sasa kwa dhamana ni 75.
  • Mfalme Zumaridi aendelea kusota rumande.

Mwanza. Kesi inayomkabili Diana Bundala maarufu kama “Mfalme Zumaridi” na wafuasi wake  93 imesomwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza huku washtakiwa wengine 34  wakipatiwa dhamana na kufanya jumla yao kufikia 75.

Washtakiwa wengine  17 wanaendelea kusota rumande pamoja na  kiongozi wao hadi kesi hiyo namba 10,11 na 12 itakapotajwa tena Machi 31, 2022.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wakili wa Utetezi, Erick Mutta kuwawasilisha barua 34  za ombi la dhamana  kwa wateja wake ambapo hakimu Monica Ndyekobora akaridhia dhamana.

Zumaridi na washtakiwa 17 wamerejshwa Gereza Kuu Butimba na wanatarajia kuungana na wenzao waliopewa dhamana  Machi 31, 2022 kesi zao zitakaposomwa tena.


Soma zaidi:

‘Mfalme’ Zumaridi kufikishwa mahakamani


Wakisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Monica Ndyekobora,  Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Doecas Ankyoo ametaja kesi hiyo na mashtaka yao ambayo ni usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili Zumaridi pekee.

Kesi namba 11  ya  shambulio la kudhuru mwili  na kuzuia maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao  inayowakabili  Zumaridi na wenzake nane huku kesi na 12 ni kusanyiko lisilokua halali inayowaweka kitanzini  Zumaridi na wafuasi wake 84.

Katika kesi hiyo, Serikali imewakilishwa na Wakili Dorcas Ankyoo ambaye aliishia kuitaja tu kesi namba 10 inayomkabiri Zumaridi pekee na kutokana na mahakama kutokuwa na mamlaka ya kisheria kuisikiliza shauri hilo Hakimu Ndyekobora akaipangia March 31, 2022.

Katika kesi namba 11 na 12, Wakili Ankyoo amesema upepelezi umekamilika na akaomba tarehe nyingine ipangwe kwa ajili ya kusikiliza hoja  za awali na hakimu Ndyekobora akaipaga March 31, 2022.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV