Kesi ya Mfalme Zumaridi yapigwa kalenda, wawili wakipata dhamana

April 14, 2022 1:54 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeahirishwa hadi Aprili 28, 2022.
  • Ni Diana Bundala na wenzake 91 wanaokabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo kusafirisha watu. 

Mwanza. Diana Bundala maarufu kama “Mfalme Zumaridi Mungu chini ya jua”, anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha binadamu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Mwanza, amebaki na wafuasi watano mahabusu kati ya 91 walioapa kukaa naye huko na kukataa dhamana siku ya kwanza walipofikishwa mahakamani.

Wafuasi hao wamezidi kupungua kwa kupata dhamana kila wanapofikishwa mahakamani na kukiuka kauli yao ya awali kwamba wapo tayari kubaki naye mahabusu kuliko kukubali kudhaminiwa.

Mpaka sasa wamebaki wafuasi watano pekee kati  ya 91 waliokataa kudhaminiwa siku ya kwanza Machi 3 mwaka huu walipofikishwa mahakamani hapo.

Wafuasi hao watano ambao dhamana zao mpaka jana zilikuwa wazi wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutokukubali kudhaminiwa kwa madai kwamba wapo tayari kufa na mfalume wao huko gerezani.

Machi 31, mwaka huu wafuasi hao walikuwa wamebaki saba, lakini jana wawili waligeuka na kukubali dhamana.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, wakili wa washtakiwa hao, Eric Mutta amesema washtakiwa hao watano bado wameendelea na msimamo wa kutokubali dhamana.

”Hawa washtakiwa bado hawajakubali sasa na mimi kama wakili wao siwezi kuwalazimisha wakubali, tunaendelea kuwashauri na siku wakikubali watadhaminiwa maana dhamana zao zipo wazi,” amesema Wakili Mutta.


Soma zaidi:


Mfalme Zumaridi anakabiliwa na kesi ya kusafirisha binadamu ambayo haina dhamana na kumfanya abaki mahabusu katika gereza la Butimba mkoani Mwanza tangu alipokamatwa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu pamoja na wafuasi wake.

Wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kushambulia na kuzuia polisi  kufanya kazi yao na kusafirisha binadamu ambalo linamkabili Zumaridi peke yake.

Mchungaji huyo akiwa mahakamani leo ameonekana akiwa na furaha na hakujifunika uso wake kama ilivyokuwa kipindi wiki zilizopita alipofikishwa mahakamani hapo akiwa amejifunika  ‘gubigubi’ kwa kitenge.

Wakili wa serikali mwandamizi, Emanuel Luvinga ameieleza mahakama hiyo kwamba waliajiandaa kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao, lakini hakimu wao amepata udhuru hayupo mahakamani.

Kutokana na hali hiyo, Wakili huyo aliomba ipangwe siku nyingine ili washtakiwa waweze kusomemewa maelezo ya awali.

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Stella Kiama aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 28, mwaka huu  kwa washtakiwa kusomewa maeleza ya awali.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV