Kinachofuata baada ya kina Mbowe kukutwa na kesi ya kujibu

February 18, 2022 1:32 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wataanza kujitetea Machi 4, 2022.
  • Wanausidia kuwa na mashahidi 22.
  • Washtakiwa hao wanakabiliwa kesi ya ugaidi.

Dar es Salaam. Baada ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuwakuta na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wataanza kujitetea Machi 4, 2022 katika kesi ya ugaidi inayowakabili.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Ling’wenya.

Leo Ijumaa Februari 18, 2022 Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo namba 217  ya mwaka 202o, amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 13 wa Jamhuri na vielelezo, mahakama imeona washtakiwa wote wanne wana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi huo mdogo, Jaji Tiganga amesema baada ya mahakama kupitia vielelezo hivyo na mashahidi vilivyotolewa kuthibitisha makosa yanayowakabili na baada ya kujiridhisha imeona washitakiwa wote wana kesi ya kujibu katika shtaka la kwanza hadi la tano.

Katika shtaka la sita, mahakama imesema hawana kesi ya kujibu kwa sababu hakukuwa na vielelezo vya kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.


Soma zaidi:


Uamuzi uliofanywa leo na Jaji Tiganga umekuja baada ya upande wa Jamhuri kukamilisha kuwasilisha ushahidi wake wiki hii kupitia mashahidi wake 13 kati ya 24 waliotarajiwa kutoa ushahidi mahakamani. 

Bada ya uamuzi huo, Wakili anayeongoza jopo la upande wa utetezi, Peter Kibatala akaiomba mahakama kuwa washtakiwa hao waanze kujitetea Machi 4, 2022.

Pande zozote mbili zimeridhia tarehe hiyo ya washtakiwa waanze kujitetea na Jaji Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 4.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV