Vunjo yaendeleza rekodi ya kukosa mbunge anayehudumu mihula miwili mfululizo

August 5, 2025 2:40 pm · Esau Ng'umbi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kila baada ya uchaguzi mkuu, jimbo hilo huibua sura mpya bungeni
  • Mpaka mwaka 2025, jimbo hilo limeongozwa na wabunge sita kutoka vyama vitatu tofauti.

Dar es Salaam. Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 1992, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro limeendelea kuweka rekodi ya kutokuwa na mbunge anayehudumu kwa vipindi viwili mfululizo. 

Uchambuzi uliofanywa na Nukta Habari umebaini kila baada ya uchaguzi mkuu, jimbo hilo huibua sura mpya bungeni, hali inayoashiria mabadiliko ya mara kwa mara katika mwelekeo wa kisiasa wa wananchi wake.

Hali hiyo imedhihirika tena mwaka huu mara baada ya mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake Charles Kimei, kushindwa kufua dafu katika kura za maoni zilizopigwa jana Agosti 4.

Kimei ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha na uchumi akihudumu katika nafasi mbalimbali ikiwemo ukurugenzi wa benki ya CRDB,  alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Vunjo mwaka 2020 lakini ameangushwa na Enock Koola katika kura za maoni mwaka 2025.

Ikiwa Kamati Kuu ya CCM itaridhia matokeo hayo na Koola kushinda kwenye uchaguzi maana yake rasmi jimbo hilo litakuwa na sura mpya.

Bado haijawa wazi juu ya nini sababu hasa ya mabadiliko haya ya kila baada ya miaka mitano kwa wakazi wa Vunjo, Je? Ni hamu ya wapiga kura kuona mabadiliko ya uongozi au viongozi  kushindwa kutimiza matarajio ya wananchi.

Mpaka sasa jimbo hilo limeongozwa na wabunge kutoka vyama vitatu tofauti ikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Labour Party (TLP) pamoja na NCCR – Mageuzi.

Kimei alipokea kijiti kutoka kwa James Mbatia wa NCCR Mageuzi aliyeongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 2015 – 2020.

Ingawa hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Mbatia kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa ndiye aliyeanza kuliwakilisha bungeni baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995.

Kutokana na migogoro ndani ya chama chake Mrema alijiunga na TLP mwaka 2000 ambako nako aligombea urais wa Tanzania na  na kushika nafasi ya tatu. Picha. Daily News

Agustino Mrema 2010 – 2015 (TLP)

Mwaka 2010 mpaka 2015 jimbo hilo lilikuwa chini ya Augustino Lyatonga Mrema wa TLP.

Mrema ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe na wenye historia ndefu nchini Tanzania.

Kwanza ndiye mgombea wa kwanza wa urais kupitia chama pinzani aliyechuana na Hayati Benjamin Mkapa kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 ambaye alipata asilimia 21 ya kura zote kupitia chama cha NCCR Mageuzi.

Kutokana na migogoro ndani ya chama chake Mrema alijiunga na TLP mwaka 2000 ambako nako aligombea urais wa Tanzania na  na kushika nafasi ya tatu. 

Mrema ni miongoni mwa wanasiasa waliowahi kuwa wabunge kupitia vyama vitatu tofauti katika majimbo tofauti, aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na baadaye Vunjo  kupitia TLP.

Hadi anafikwa na umauti Agosti 21, 2022 alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya msamaha kwa wafungwa, maarufu bodi ya Parole.

Aloyce Kimaro  2005 – 2010 (CCM)

Kwa mara ya kwanza Chama cha Mapinduzi kilishinda Jimbo la Vunjo kupitia Aloyce Kimaro aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 mpaka 2010.

Kimaro alichukua jimbo hilo kutoka kwa Meja Jesse Makundi aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya Chama cha TLP kuanzia mwaka 2000 mpaka 2005.

Mbali na kuwa mbunge  Makundi aliyefariki dunia Agosti 23, 2021, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa TLP mwaka 2010/11  aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Mwika Kaskazini 2010 -2015 na mwaka 2019 aligombea nafasi ya mwenyekiti kijiji nafasi ambayo hakupata.

James Mbatia 1995 – 2000 (NCCR)

Jina la James Mbatia siyo geni miongoni mwa Watanzania hususani Jimbo la Vunjo kwani ndiye alikuwa Mbunge wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.

Mwaka 1995 katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Vunjo ilichagua mbunge kutoka NCCR Mageuzi wakati huo akiwa kijana wa miaka 31 tu.

Mbatia alipata ushindi mkubwa wa asilimia 83.9 (kura 57,714) huku mgombea wa CCM, Msaki Leonard akipata asilimia 9.4 (kura 6,468). 

Sokomoko ndani ya NCCR Mageuzi lilidhoofisha siasa za siku za mbele za Mbatia katika Jimbo la Vunjo. 

Augustine Mrema alipohamia TLP mwaka 2000 ikiwa na ushawishi  mkubwa wa kisiasa,  akampigia debe mgombea wa TLP badala ya Mbatia wa NCCR.

Kutopigiwa debe na Mrema pale Vunjo mwaka 2000 kuliathiri safari ya kisiasa ya Mbatia na aliangushwa kwenye uchaguzi huo na mgombea wa TLP, Jesse Makundi ambaye aliongoza Vunjo tokea mwaka 2000 – 2005.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
21 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV