Viwango vya kubadili fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania

November 21, 2024 9:48 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Shilingi ya Tanzania yazidi kuimarika siku baada ya siku dhidi ya Dola ya Marekani. Ndani ya mwezi Novemba kulinganisha na mwezi uliopita ambapo Dola ilikuwa juu zaidi.

Kuimarika kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani ni shangwe kwa wafanyabiashara hasa wanaoagiza bidhaa nje ya nchi, kwasababu hutumia Dola kufanya malipo za bidhaa zao.

Hata katika soko la rejareja kutoka benki za biashara, shilingi imeimarika, viwango cha kubadili fedha (exchange rate). Benki ya NMB PLC vinabainisha kuwa Dola moja inauzwa Sh2,710 leo kutoka Sh2,740 mwezi mmoja uliopita.

Katika soko la jumla pia shilingi imeonekana kuipunguza makali Dola ya Marekani. Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) shilingi ya Tanzania imepanda thamani kwa Sh75.36 kulingana na tofauti ya bei ya kununua iliyopo leo na ile ya mwezi uliopita.

Tumia viwango hivi kuuza na kununua Dola kwa Shilingi ya Tanzania leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks