Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Desemba 30, 2024

December 30, 2024 10:57 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Ndani ya mwezi Disemba thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya Dola ya Marekani iliyokuwa ikinunuliwa kwa Sh2,608 na kuuzwa Sh2,634 Disemba 2, 2024.

Thamani ya Dola ya Marekani ilishuka zaidi Disemba 13, hadi kufikia Sh2,298, bei ambayo ni kiwango chini zaidi kurekodiwa ndani ya mwaka huu.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba, amesema kuwa kupanda kwa thamani ya shilingi kunatokana na mambo mbalimbali, ikiwemo kuimarika kwa uchumi wa Marekani na kushuka kwa viwango vya riba nchini humo. Hali hii imevutia wawekezaji kuelekeza mitaji yao katika masoko mengine, hivyo kuongeza upatikanaji wa dola za Marekani kwenye soko la kimataifa.

Ndani ya kipindi sawa cha mwezi mmoja, bei ya dhahabu pia imeshuka kwa Sh675,153, ambayo ni sawa na upungufu wa takriban asilimia 9.74, kutoka Sh6,929,631 milioni iliyokuwa ikitumika kununua Disemba 2 hadi Sh6,254,478 inayotumika kununua leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks