Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Desemba 31, 2024
Dar es Salaam. Thamani ya Shilingi ya Tanzania imeshuka kidogo kwa Sh1 dhidi ya Dola ya Marekani, ambayo leo inanunuliwa kwa Sh2,382 na kuuzwa kwa Sh2,406. Hali hii ni tofauti na jana, Desemba 30, 2024, ambapo Dola ilipatikana kwa Sh2,381 kununua na Sh2,405 kuuza.
Kwa wastani wa mwezi mzima kutoka Desemba 1, Dola ya Marekani imekuwa na thamani ya Sh2,394.75, kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Kwa waliohifadhi fedha za kigeni, kushuka kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania kunatoa fursa nzuri ya kubadilisha fedha hizo, kwa sababu mabadiliko ya hivi sasa yanawapa faida zaidi kutokana na kiwango cha juu cha ubadilishaji wa Dola ya Marekani.
Bei ya dhahabu imeendelea kushuka, kutoka jana ilipokuwa ikinunuliwa kwa Sh6,254,478 imepungua kwa Sh9,789 na leo kununuliwa Sh6,244,689.