Dola ya Marekani yapaa kwa Sh5 dhidi ya Shilingi ya Tanzania Mei 19, 2026

May 19, 2026 10:06 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 0.19 kwa bei ya kuuza na kununua ukilinganisha  bei iliyotumika jana Mei 18, 2026 ambapo dola iliuzwa kwa Sh2,650 na kununuliwa kwa 2,570.

Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania ikiongezeka thamani kwa Sh5 ndani ya siku moja kwa bei ya kuuza na kununua katika benki za kibiashara za NMB na CRDB.

Kwa mujibu wa takwimu za viwango vya kubadilisha fedha katika benki hizo mbili vinavyotumika leo Mei 19, 2026, Dola ya Marekani inauzwa kwa Sh2,655 na kununuliwa kwa Sh2,575 katika benki hizo.

Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 0.19 kwa bei ya kuuza na kununua ukilinganisha na bei iliyotumika jana Mei 18, 2026 ambapo dola iliuzwa kwa Sh2,650 na kununuliwa kwa 2,570.

Hii inamaanisha kuwa gharama za uagizaji wa bidhaa kutoka nje kama mafuta na bidhaa nyingine muhimu zitaongezeka hali inayoweza kuchochea mfumuko wa bei na kuongeza mzigo kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje ya nchi.

Hali kama hiyo pia nimeonekana katika sarafu nyingine kama vile Pauni ya Uingereza, Euro pamoja na Yuani ya China huku sarafu za kikanda kama vile Shilingi ya Kenya na Uganda vikiimarika kiduchu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV