Uviko-19 wachangia kukatisha uhai wa watoto milioni 5 duniani

January 11, 2023 5:53 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Takriban watoto milioni 5 walikufa kabla ya kusherehekea mwaka wao wa tano wa kuzaliwa mwaka 2021.
  • Kutatizwa kwa mifumo ya afya kulikosababishwa na Uviko-19 kwatajwa kama sababu.
  • Watoto wengine milioni 2.1 pamoja na vijana wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 24 walikufa mwaka 2021.

Dar es Salaam. Takriban watoto milioni 5 walikufa kabla ya kusherehekea mwaka wao wa tano wa kuzaliwa huku wengine milioni 2.1 pamoja na vijana wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 24 walikufa mwaka 2021.

Sababu mojawapo ni janga la Uviko-19 lilichangia kuvurugwa kwa utoaji wa huduma za afya za uhakika kwa watoto na vijana. 

Hiyo ni kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni zaidi yaliyotolewa na kundi la mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofuatilia vifo vya watoto (UN IGME) kupitia taarifa yao iliyotolewa Januari 10, 2022 Marekani pamoja na Geneva, Uswisi. 

Mbali na makadirio hayo mapya, ripoti nyingine ya kando ya kundi hilo imebaini kuwa katika kipindi hicho hicho, watoto milioni 1.9 walizaliwa wafu. 

“Idadi kubwa ya vifo hivi vingaliweza kuzuiwa kwa kuhakikisha kuna upatikanaji sawa wa huduma bora za afya na zenye ubora wa juu kwa wajawazito, watoto wachanga na vijana  barubaru,”  amesema Vidhya Ganesh, Mkurugenzi wa Idara  ya Uchambuzi wa Data, Mipango na Ufuatiliaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Kila siku, wazazi wengi zaidi wanakumbwa na kiwewe na msongo wa kupoteza watoto wao, na wakati mwingine hata kabla ya pumzi yao ya kwanza. 

“Kusambaa kwa janga hilo linaloweza kuzuilika hakupaswi kukubalika. Maendeleo yanawezekana ikiwa kuna utashi wa kisiasa na uwekezaji unaolenga sekta hiyo kuhakikisha huduma ya afya ya msingi inapatikana kwa kila mama na kila mtoto,” amesema afisa huyo wa UNICEF. 

Await Said anamwangalia mjukuu wake mchanga Ayah, ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kichocho na uzito wa kilo 1.3 tu, kwani yuko kwenye incubator katika Hospitali ya Ualimu Juba, Juba, Sudan Kusini. Picha | UNICEF/UN0159228/Naftalin.

Uviko-19 watajwa

Licha ya kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja Uviko-19 na vifo vya watoto na vijana miaka ya hivi karibu, ripoti hiyo imeeleza kuwa kutatizwa kwa mifumo ya afya na uchumi kutokana na janga hilo kwa kiasi fulani kumechangia matokeo hasi kwa afya za watoto. 

Pia kuvurugwa kwa ratiba za kampeni za chanjo, huduma za lishe na kupata huduma za msingi za afya, vitu ambavyo vitahatarisha afya na ustawi wao kwa miaka ijayo. 

Kuna ahueni

Hata hivyo, ripoti hiyo inaonyesha matokeo chanya na hatari ndogo ya vifo miongoni mwa watu wa umri wote tangu mwaka 2000.

Vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa asilimia 50 tangu kuanza kwa karne hii ya 21, huku vifo vya watoto wakubwa na vijana vilipungua kwa asilimia 36 na vifo vya watoto wachanga tumboni vilipungua kwa asilimia 35. 

Hii ilifanikishwa na uwekezaji zaidi uliokuweko katika kuimarisha mifumo ya afya ya msingi ikilenga wanawake, watoto na vijana. 


Soma zaidi


Hata hivyo mafanikio yote hayo yaliporomoka tangu mwaka 2010 na nchi 54 zitashindwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu kuhusu watoto wenye umri wa chini ya miaka 5. 

“Iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuimarisha huduma za afya, takribani watoto milioni 59 na vijana watakufa kabla ya kufikia mwaka 2030 na takribani watoto milioni 16 watazaliwa wakiwa tayari wameshakufa,” yameonya mashirika hayo. 

“Inasikitisha sana kuwa fursa ya mtoto kuishi inatokana na pahali alipozaliwa, na kwamba kuna ukosefu mkubwa wa uwiano kwenye fursa yao ya kupata huduma za afya,” amesema Dk Anshu Banerjee, Mkurugenzi wa huduma za wajawazito, watoto wachanga, watoto na vijana barubaru katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO). 

Amesema watoto kokote waliko wanahitaji mifumo thabiti ya afya ya msingi, ikikidhi mahitaji yao na ya familia zao ili kokote pale walikozaliwa wana fursa nzuri ya kuanza maisha na wana matumaini ya siku zao usoni. 

“Ingawa nchi hizo za Afrika zina asilimia 29 ya vifo vyote hai duniani kote, ukanda huo wa Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara linabeba asilimia 56 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa mwaka 2021,” imesema ripoti hiyo huku zile za kusini mwa Asia zikiwa na asilimia 26. 


Tangazo


Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV