Uviko-19: Mambo yatakayosaidia kuepuka matatizo ya akili

October 11, 2022 1:40 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Watanzania milioni 7 wanaishi na matatizo ya afya ya akili.
  • Bima ya afya, ushirikiano wa wadau, na mtazamo mpya kusaidia utatuzi.
  • Ukatili na udhalilishaji ni miongoni wa sababu kuu.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa dunia inatakiwa kutoa kipaumbele kushughulikia tatizo la afya ya akili wakati huo ambao inakabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo Uviko-19.

WHO imeeleza kuwa tatizo hilo limeongezeka kwa zaidi ya asilimia 25 ndani ya mwaka mmoja tangu kulipotiwa kisa cha kwanza mwaka 2019, jambo lililoathiri zaidi maisha ya watu. 

Shirika hilo limesema mtu mmoja kati ya watu nane ana tatizo la ugonjwa wa akili, huku Tanzania ikikadiriwa kuwa na watu milioni 7 wenye tatizo hilo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliyekuwa akizungumza katika kongamano la afya ya akili jana Oktoba 11, jijini Dar es Salaam amesema matatizo ya akili yanayowakumba zaidi Watanzania ni sonono, kihoro na ulevi wa kupindukia.

Suluhu ya tatizo

Ili kuhakikisha tatizo hili linapatiwa ufumbuzi inabidi kuukubali na kukabili uhalisia wa tatizo hili na kuanzisha utoaji wa huduma nafuu na bora zinazojikita katika kuepusha magonjwa ya akili.

WHO inashauri kuwa ni lazima tuongeze thamani na dhamira tunayotoa kwa afya ya akili kama watu binafsi, jumuiya na serikali na tulingane na thamani hiyo na kujitolea zaidi, ushirikiano na uwekezaji wa washika dau wote, katika sekta zote. 


Soma pia

Huduma za afya zinahitajika kuweka msisitizo zaidi kwenye upatikanaji wa kinga kujiepusha na ongezeko hili la kasi na kupunguza gharama pamoja na matokeo mabaya ya matatizo ya akili.

“Tulikubali tatizo hili katika nchi yetu lakini kubwa tujikite kwenye kukinga zaidi, kipi tunaweza kufanya kama jamii kuhakikisha kinga inapatikana na kutibu mahitaji ya sasa ya afya ya akili,” Waziri Mwalimu alisema.

Sambamba na hayo jitihada za uwekezaji na kuwapata wataalamu wa magonjwa ya akili katika ngazi za chini za utoaji wa huduma na kujumuishwa kwa huduma za afya ya akili kwenye bima kutasaidia kupatikana kwa tiba.

WHO inaeleza kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa tatizo hili ambalo hivi sasa ni kutokuwa na usawa wa kijamii na kiuchumi, dharura za afya ya umma, migogoro ya muda mrefu.

“Afya ya akili ni eneo ambalo halivutii wadau wengi, ni kutokana na unyanyapaa. Tukizungumza afya ya akili tunaonekana sisi wote ni wagonjwa wa akili, na ndiyo tatizo linaloikumba nchi hii…bila afya ya akili hakuna afya,” alisema Ummy.

Sababu nyingine za kuzidi kwa magonjwa ya akili ni kuongezeka kwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kama ubakaji na kulawitiwa kwa watoto.

Pia kushindwa kutimiza matarajio ya mafanikio, mambo ya mahusiano, ukosefu wa fedha, magonjwa ya muda mrefu na matatizo ya kifamilia yasipotatuliwa husababisha magonjwa ya akili.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV