Usomaji vitabu bado bado Tanzania

November 15, 2022 12:03 pm · Abdushakur
Share
Tweet
Copy Link
  • Wasomi wasema watu wanakosa maarifa kwa sababu hawasomi.
  • Waanza kutoa hamasa kuongeza idadi ya wasomi.
  • Serikali yakarabati maktaba kuvutia watu kusoma vitabu. 

Mwanza. Elimu ikiwa ni msingi mkuu wa maendeleo kwa taifa lolote ulimwenguni, Watanzania wameaswa kujenga utamaduni wa kusoma vitabu kupata maarifa yaliyohifadhiwa kwa njia ya maandishi.

Balozi Ombeni Sefue ametoa rai hiyo akiwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kigoda cha Uprofesa cha Hayati Rais Benjamin Mkapa lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT) kampasi ya Mwanza, Jumamosi Novemba 12, 2022.

“Hayati Mkapa alipenda kusoma vitabu na majarida kuliko kutumia muda wake mwingi kupiga domo kuhusu mambo yasiyo na msingi au vikao vya kupewa sifa,” amesema Balozi Sefue. 

Balozi Sefue amebainisha kuwa utaratibu wa kusoma vitabu humfanya msomaji kuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kupata mawazo mapya ambayo hayakuwepo hapo awali.

Akimtolea mfano Hayati Mkapa aliyesifika kwa kujenga hoja imara kwenye makongamano na mijadala mbalimbali, Balozi Sefuye amesema kuwa hayo ni miongoni mwa matunda ya utamaduni wa kusoma vitabu.

Uimara wa falsafa za Hayati Mkapa ukijengwa na utaratibu wa usomaji wa vitabu mbalimbali, Mwanafalsafa na mhadhiri wa SAUT Innocent Sanga amesema kuwa kiongozi huyo alikuwa na msimamo katika hoja zake.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amefafanua kuwa Hayati Mkapa alisifika kwa mawazo chanya kufuatia ufatiliaji wake wa mambo muhimu yaliyojificha katika maandishi. 

Utamaduni wa kusoma vitabu umetajwa kuwa  changamoto kwa kizazi cha sasa ambapo kundi kubwa hawana kuhusu suala hilo.

Washiriki wa Kongamano la Kigoda cha Uprofesa cha Hayati Rais Benjamin Mkapa lililofanyika mkoani Mwanza Oktoba 12, 2022. Picha | Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Hali ya usomaji wa Vitabu

Leah Ibrahim Mkazi wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza katika mahojiano na Nukta Habari (www.nukta.co.tz) amesema kuwa hupendelea kusoma vitabu vya dini kama Biblia akiamini kuna mafundisho mengi ila hufanya hivyo wakati wa ibada pekee.

Mkazi mwingine Victor Godfrey Lusega amesema tangu amalize elimu ya sekondari hakumbuki mara ya mwisho kusoma kitabu chochote kwani muda wake mwingi anatumia kutafuta riziki.

Hili ni tofauti kwa Oppa Ezekiel Choga ambaye hupenda kusoma vitabu mara kwa mara kutokana na hamu yake ya kujifunza misamiati mipya na kupata mawazo chanya kufikia maendeleo.


Soma zaidi:


Sababu za watu kutopenda kusoma vitabu

Mwanasaikolojia na Mhadhiri SAUT Leons Maziku amesema baadhi ya watu hupenda njia ya mkato kufikia mafanikio na hatimaye hukosa hamasa ya kutafuta vitu muhimu vilivyohifadhiwa kwenye maandishi. 

“Tatizo watu wengi wanapenda short cut way (njia ya mkato) ili kufanikiwa, kila kitu kina njia yake ya mafanikio na nidhamu ya mafanikio lazima uwe nayo,”  amesema Maziku.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dk Aneth Komba   katika tamasha la 13 la kimataifa la vitabu Tanzania lilofanyika Oktoba 11 hadi 15  mwaka huu, alisema kuwa hamasa bado ni ndogo kwa jamii kushiriki usomaji wa vitabu mbalimbali. 

“Tunashirikina  na  kuhamasisha ari mpya ya usomaji na tutaendelea kuhimiza ari ya usomaji wa vitabu, tusome vitabu vyote kwa ajili ya kupata maarifa,’’ alisema Dk Komba.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Waziri Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2022/23, alisema kuwa Serikali imeanza kujenga utamaduni wa kusoma vitabu kwa kuanza na wanafunzi.

Prof Mkenda alieeleza kuwa wizara imeanza kwa kugawa vitabu shuleni ili kuwajengea utamaduni wanafunzi kujisomea wakiamini ndiyo taifa la kesho.

Wizara yake ilitoa ushauri wa kitaaluma katika vituo 286 kati ya 350 vya huduma ya maktaba na kuboresha maktaba za mkoa ikilenga kuongeza idadi ya wanaosoma vitabu nchini.

Prof. Mkenda alisema kuwa takriban Sh1 bilioni zimetengwa kufadhili uzalishaji wa vitabu kwa mwaka wa fedha 2022/23 ili kuhamasisha Watanzania kusoma kwa wingi vitabu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV