Usidanganyike: Bidhaa za usafi hazitibu Corona

July 30, 2020 4:27 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bidhaa hizo ni zile zinazotumika kuondoa uchafu kwenye vifaa, vitu na maeneo ya nyumba.
  • Bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya mwili na hazitibu Corona. 
  • Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshauri bidhaa hizo kuwekwa mbali na watoto.

Dar es Salaam. Ugonjwa wa Corona umezua mengi ukiwemo uzushi kuhusu matumizi ya bidhaa mbalimbali ambazo zinadhaniwa kutibu ugonjwa wa virusi vya Corona.

Baadhi ya watu wameibuka na kudai kuwa bidhaa zinazotumika kuondoa uchafu kwenye vifaa mbalimbali (bleach na disinfectants) zinaweza kumsaidia mtu kuishinda corona pale anapokunywa au kupulizia mwili.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeweka wazi kuwa bidhaa hizo ni kwa ajili ya kusafisha vifaa, ngua na maeneo mbalimbali ya nyumba na siyo kwa matumizi ya mwili wa binadamu kwa kunywa au kujipulizia.


Zinazohusiana:


WHO imesema kama zitatumika kinyume na matumizi zinaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu na kuongeza kuwa hazitibu ugonjwa Corona.

“Kwa namna yeyote ile, usipulizie au kutumia “bleach” au “disinfectants” chochote kwenye mwili wako. Vitu hivi vinaweza kuwa sumu pale vitakapotumika kama kinywaji na kusababisha muwasho kwenye ngozi na macho,” imesema WHO. 

Pia dawa hizo zinatakiwa kuwekwa mbali na watoto ili kuepusha kunywa, jambo litakalowaweka katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV