Matumaini mapya: Nusu ya wanafamilia waliokatwa miguu kwa “ugonjwa wa ajabu”

February 16, 2023 7:11 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Wapatiwa miguu ya bandia na kuendelea na shughuli za uzalishaji.
  • Ni watu saba kati ya 14 waliokatwa miguu kwa ugonjwa wa jabu.
  • Wasema kwa sasa hali nishwari baada ya kusaidia na wasamaria wema. 

Mwanza. Huzuni na majonzi hayapo tena. Hivi ndivyo unavyoweza kumuelezea Amina Kalazi (62) mkazi wa mkazi wa kijiji cha Igayaza wilayani Muleba mkoani Kagera. 

Kwa takribani miongo mitatu mfululizo maisha ya Amina Kalazi (60) mkazi wa kijiji cha Igayaza wilayani Muleba yalikuwa yakitawaliwa na machozi baada ya familia yake kukumbwa na ugonjwa uliofanya sehemu kubwa ya familia yake kukatwa miguu.

Amina, mama wa watoto 14, alizaliwa mzima akiwa na viungo vyote vya  mwili lakini historia ya maisha yake imebadilika baada ya kujikuta yeye na watoto wake saba kupoteza viungo vya miguu yote miwili kutokana na “ugonjwa wanaouita wa ajabu”.

Mbali naya na watoto wake, watu wanne kutoka kwenye ukoo upande wa mama yake Amina nao walishakatwa miguu.

Kukatwa kwa miguu kwa ndugu hao wa familia moja kuliwafanya wapate ulemavu wa kudumu kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

Mbali na ulemavu, familia ilijikuta kila kipindi ikisaka fedha kwa ajili ya kuwatibu ndugu walioanza kupata ugonjwa huo.

Kwa sasa majonzi hayapo tena kama wanavyosema Waswahili kuwa “hakuna tatizo linalodumu milele”

Tofauti na zamani kwa sasa familia hiyo inaendelea vizuri baada ya wasamaria wema kuwapatia miguu bandia inayowasaidia kutembea na kufanya shughuli zao za kila siku.

Akizungumza na Nukta habari (www.nukta.co.tz) kwa njia ya simu, mmoja wa wanafamilia hapo, Faridi Omary anasema mpaka sasa hakuna mtu mwingine kwenye familia hiyo ambaye amekumbwa na ugonjwa huo.

“Hatujapata kesi kama hiyo tena familia inaendelea vizuri na kila mmoja anaendelea na shughuli zake,” anasema Faridi ambaye mtoto wake Husna (10) anaendelea na masomo yake katika Shule ya Msingi Mgeza Mseto iliyopo Bukoba ambapo kwa sasa yupo darasa la nne.

Kutokana na miguu yao kukatwa hulazimika kutembea kwa kutumia magoti huku wakishindwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato. Picha | Mariam John.

Kuhusu ndugu wengine waliokumbwa na kadhia hiyo, Faridi anasema nao walipatiwa msaada na wasamaria wema akiwemo Mkurugenzi wa taasisi ya Nitetee Foundation, Flora Lauwo ambaye aliwasaidia kujenga nyumba ya vyumba vitatu na kuwanunulia magodoro ya kulalia.

Mkurugenzi huyo alisaidia kuhakikisha watu wawili ambao miguu yao ilikatwa kufikia usawa na magoti kupatiwa miguu bandia ili iwasaidie kutembea na kuendelea na shughuli zao.

“Kwa sasa walisharudi Misenyi na wanaendelea tu vizuri tunashukuru sana Watanzania kwa msaada waliotupatia,” anasema Faridi.

Hali ilivyokuwa awali

Kwa mujibu wa Amina, ugonjwa huo huanza kwa kidole kimoja kuwasha kama funza tatizo ambalo huambatana na maumivu makali kama mtu anayeungua na moto. 

Baada ya siku chache ugonjwa husambaa kwenye vidole vyote na hubadilika kwa haraka na kusinyaa. Baadaye ngozi hubadilika rangi na kuwa nyeusi huku nyama za miguu pamoja na mifupa hushikana pamoja na kukauka.

“Tatizo hilo husambaa kwa haraka sana mifupa na nyama hushikana na kukauka kabisa na kuoza…kadiri siku zinavyoenda ugonjwa hupanda kuelekea juu ya magoti,” anasimulia Amina.


Soma zaidi: 


Hadi kwa watoto

Rahma Mathias binti wa Amina ambaye amepatiwa matibabu na mguu wa bandia bado anakumbuka namna alivyofanyiwa upasuaji wa kukatwa miguu mara tatu akiwa una ujauzito wa  miezi nane na hata baada ya kujifungua. 

“Nilianza kwa kuwashwa kama funza nilipomtumbua baadaye nilishtukia malengelenge  kama nimeungua na moto,  siku chache baadae miguu ilibadilika rangi na kuwa myeusi huku nikipata maumivu makali sana, ” alisema mwaka 2021 alipotembelewa na Nukta Habari akiwa mkoani Mwanza na kuongeza; 

“Tatizo hili lilinitesa na hata waliponipeleka hospitali  ya wilaya daktari alinieleza mishipa haipeleki damu kwenye vidole hivyo inatakiwa kukatwa.”

Licha ya kufanyiwa upasuaji bado alihisi maumivu makali yaliyosababisha ashindwe kupata usingizi. Wapo waliomshauri awe anaweka miguu kwenye maji.

Alisema wakati anafikishwa hospitali daktari alibaini mishipa haipeleki damu kwenye vidole vyote viwili na imekauka kabisa hivyo hakuna namna yoyote zaidi ya kukatwa.

Kufahamu kwa undani kisa cha wanafamilia hao kukatwa miguu, tazama video hii 

                           


Tangazo

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV